Na Ally Changwila

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), imetoa zawadi mbalimbali katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha New Life kilichopo Kigogo jijini Dar Es Salaam.

Zawadi hizo ambazo ni pamoja na mchele , sukari , mafuta na biscuit ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa TCAA ambayo licha ya kuhakikisha kuwa Anga ya Tanzania inaendelea kuwa salama pia hutoa sehemu ya mapato yake kufurahi kwa pamoja na watoto wanoishi katika mazingira magumu ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii .

Akipokea msaada huo kutoka TCAA, Mkurugenzi wa Kituo hicho Bibi Mwanaisha Magambo aliishukuru sana TCAA kwa kitendo hicho cha kuwajali watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Kwa mujibu wa Bibi Magambo kituo hicho hivi sasa kina jumla ya watoto 103, miongoni mwao wakiwemo wasichana 38 na wavulana 65 wenye umri kati ya miaka 3 na 21, waliopo katika hatua mbali mbali za masomo kuanzia msingi hadi vyuoni.

Aliongeza kuwa changamoto anayokumbana nayo sana kituoni hapo ni Elimu na Matibabu na kutoa wito kwa wenye moyo wa kukisaidia kituo hicho kujitokeza.

Bibi Magambo alisema Kituo cha New Life kilianzishwa mwaka 1998 na kutambuliwa rasmi kwa kupata usajili wa Serikali mwaka 2009 na sababu ya kuanzisha kituo hicho ni mapenzi yake ya kupenda watoto pamoja na moyo wake wa kutaka kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.Bibi Magambo ni mama wa watoto saba wote wa kiume na hivi sasa wanajitegemea .
Bibi Mwanaisha Magambo (Kushoto), Mkurugenzi wa kituo cha New Life akipokea zawadi kutoka kwa Bw.Ally Changwila Afisa Habari Msaidizi kutoka TCAA.Wengine pichani ni wawakilishi kutoka TCAA pamoja na baadhi ya watoto wanaoishi kituoni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...