Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu za mkononi milioni tatu tu mwaka 2000 hadi kufikia laini 28,000,000.
Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.
Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo.
Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.
Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.
-1.png)
Leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.
Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na mengineyo. Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri.
Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.
Watanzania KIDIJITALI zaidi!
ReplyDeleteMwaka 2000 Laini za Simu 3 Mil. tu
Mwaka 2013 Laini za Simu 28 Mil.
Nikuwa kwa sasa zaidi ya nusu ya Watanzania wanafikika Kidijitali, hivyo hiyo ni fursa nzuri sana kwa mambo ya Kimaendeleo kama haya hapa chini:
1.e-Government:
Inahitajika Serikali imfikie mwananchi Kimtandao kuanzia ngazi ya Serikali za Mitaa ili kuainisha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Mtawa na Mtawaliwa ili mambo kuwa.
2.e-Administration:
3.e-Commerce:
Kukuza na kuunganisha wigo wa mauzo ili kujenga Uchumi.
4.e-Business:
Kukuza na kuunganisha wigo wa Kibiashara ili kujenga Uchumi.
5.e-Market:
Kukuza wigo na kuunganisha Mfumo wa Masoko ya Bidhaa,Huduma hadi mitaji ya Hisa kwa njia ya Dijitali na kuamsha kazi ya mauzo na manunuzi (DOMESTIC CONSUMPTION) kati ya masoko na wanunuzi (HOUSE HOLD to INDUSRTY/FIRM) hivyo mzunguko wa Uchumi kuimarika na Uchumi kukua Ukubwa wake kwa kasi ya juu.
6.e-Health:
Kuunganisha huduma za afya ya jamii na Umma kati ya Watoa huduma na Madakitari hadi kwa Umma hivyo kuvunja Uwiano tete (DOCTOR POPULATION RATIO) kwa kuwa Idadi ya Madakitari haiwiani na idadi ya watu ktk nchi nyingi ta Kusini mwa Jangwa la Sahara, ili kuinua Hali bora ya Maisha kwa huduma za afya kwa kuwa Dakitari mmoja ataweza kuwafikia wengi zaidi kwa njia ya Mtandao kuliko ilivyo kuwa kabla na kuzaa udumavu wa kimaendeleo.
7.e-Finance:
Kutokana na No.3.e-Commerce, No.4.e-Business, na No.5.e-Market panazaliwa e-Finance itakayo wezesha Mfumo wa Malipano kutoka kwenye Uchumi na Benki kuu kuwezekana kufikika hivyo Mfumo wa Malipano wa Taifa (NATIONAL PAYMENT SYSTEM) kuimarika na kutoa fursa ya kukuza Uchumi na kuleta maendeleo.
KEY ECONOMIC PLAYERS:
HOUSEHOLD+FIRM+GOVERNMENT
Hii ni hatu nzuri sana ktk kupiga hatua za maendeleo nchini Tanzania kwa kuwa Kitaaluma ni kazi ngumu kwa Mamlaka kuufikia Umma isipokuwa kupitia hili daraja au gari la Dijitali (DIGITAL VEHICLE) kwa njia ya KEY ECONOMIC PAYERS HAPO JUU hilo linawezekana!