Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza tangu bodi hiyo kuteuliwa ambapo kilijadili mambo mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji nchini. (Picha na Francis Dande)
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya maazimio ya bodi hiyo kuhusu sera ya uwekezaji nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa kikao cha kwanza tangu bodi hiyo iteuliwe. Kushoto ni mjumbe wa Bodi hiyo, Arnold Kileo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza.
---------------------------------------------
SERIKALI imetakiwa kusitisha mara moja mpango wake wa ugawaji wa leseni za vitalu vya gesi hadi hapo itakapopatikana sera ya gesi ili kuwapa fursa watanzania kumiliki vitalu hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi, alisema kuwa endapo ugawaji wa vitalu hivyo utafanyika Oktoba mwaka huu kama ilivyopangwa, watanzania hawatakuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali hiyo.
Dk. Mengi ambaye alikuwa akizungumzia maazimio ya bodi hiyo iliyokutana mara ya kwanza jana tangu ilipoteuliwa hivi karibuni, alisema wakati Serikali iko mbioni kufanya mnada wa vitalu hivyo saba vya gesi, hakuna kipengere kinachomwezesha mtanzania kumiliki gesi hiyo.
Akizungumzia sera za uwekezaji kwa ujumla, Dk. Mengi alisema taasisi hiyo inaitaka Serikali kuingiza kwenye Katiba mpya inayokuja kipengere kinachowapa haki watanzania kuwa na ubia na wawekezaji wa nje badala ya kuwaachia wageni hao kumiliki rasilimali za hapa nchini kwa asilimia 100.
Alisema hali hiyo itawawezesha watanzania kuwa na hali ya kumiliki na kulinda rasilimali zao ambazo kwa sasa zinawanufaisha zaidi wageni kuliko watanzania wenyewe.
“Sisi tunaitaka Serikali ihakikishe kuwa shughuli yoyote ya uwekezaji wa kiuchimi, iwe na mtanzania ndani yake na watanzania hawa, wasishindwanishwe na wawekezaji wakubwa wan je,” alisema Dk. Mengi.
Naye Makamu mwenyekiti Salum Shamte, alisema kuwa Serikali inapaswa kuhakikisha sheria ya manunuzi za umma inawanufaisha zaidi watanzania kuliko wawekezaji.
Alisema hivi sasa kiasi kikubwa cha fedha za Bajeti ya kila mwaka, zinatumika katika kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma na kazi hiyo imekuwa ikifanywa na wawekezaji badala ya kuwawezesha watanzania.
Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Dk. Mengi alisema kuwa asilimia 80 ya Bajeti ya mwaka huu wa fedha, itatumika kwa ajili ya manunuzi ya umma hivyo ni vyema kazi hiyo ikafanywa na watanzania.
“Ukiangalia bajeti ya mwaka huu, karibu asilimia 80, sawa na sh trilioni 14 zitatumika kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma za umma. Fedha hizi zikiingia kwa watanzania, zitachangia sana kukuza uchumi wa taifa,” alisema Dk. Mengi.
Ni Mr. KILEWO sio Kileo
ReplyDeleteMasuala ya rasilimali za taifa kama gesi, madini na wanyama pori yanatakiwa kujadiliwa na bunge ili kutoa muongozo kwa Serikali kabla kuendelezwa. Wenzetu Uarabuni wametajirika kwa mafuta yao, wengi wanamiliki visima vya mafuta lakini sisi Waafrika na hususani watanzania madini yanachimbuliwa na nakuchukuliwa na wageni sisi hali tukibakia masikini.Kunawakati wazungu wamekuwa wakitutkana waafrika kuwa waafrika hawana upeo mkubwa wa kufikiri, wamefanya tafiti mbalimbali kuthibitisha hilo, ebu sasa watanzania tuthibitishe kwa vitendo japo kwa kudhibiti kuibiwa mali zetu huku tunaona. Suala la wawekezaji tulazimishe kila investment inayotoka nje ihusishe mtanzania kupitia Joint Ventures na si vinginevyo.
ReplyDeleteNi mimi mkereketwa wa Rasilimali za Taifa kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.
Mengi umepewa vitalu vingi sana kwenye madini ambavyo hadi leo ujaviendeleza sasa kwenye gesi utaka uingie pia? oil and gas in a capital intensive industry hamna na narudia hamna mtanzania mwenye uwezo wa kushinda na BG/STATOIL ETC. hii tabia ya kulialia na kuombaomba vya bure inabidi iishe.
ReplyDeleteHata Ethiopia kwa mfano kuna sera ya kulazimisha mwekezaji kufanya kazi na mzawa kwa asilimia 50 kwa 50 Serikali inafungu la fedha kukopesha wazawa wanaothubutu kuwekeza kama wawekezaji wenza. Tuwezeshe wazawa ili mapato yabaki na kuendeleza ndani.
ReplyDeletewazawa wanatakiwa kupewa kipaumbele zaidi kuliko wageni,na tusione wivu juu ya hili ,wenyeji mbele wageni nyuma ,hapo ndio nchi itaenda ,mbele la sivyo wageni wakipewa kipaumbele watachukua kila kitu na wataenda kujenga kwao ,vinaja wanakosa ajira kwa kuwa hapo kwetu asilimia kubwa wote wanategemea ajira serikalini,sasa kukiwa na makampuni ya wazawa wataajiliwa wazawa tena,japo ,hapo nyumbani kuna matatizo ya ukabila,udini,ukanda kwenye suala la ajira,cha msingi ni kusimama pamoja tu na si vinginevyo.
ReplyDelete