IMG_1445
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akielezea jukumu lao kubwa wao kama Unic ni kuelimisha jamii ambapo kwa kufanya hivyo wamehamasika kuanzisha vilabu vya kujisomea kwa shule za msingi vitakavyowajengea watoto msingi mzuri wa kupenda kujisomea ili kufahamu mambo mengi zaidi yanayoendelea duniani katika nyanja ya Sayansi, Teknolojia na habari.
IMG_1488
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha ( wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga ( wa nne kushoto) wakikabidhi vitabu vya kujisomea kwa walimu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa kushirkiana na Soma Book Café walihamasisha kuanzishwa kwa Klabu za Kujisomea katika shule tatu za msingi ambazo ni Hananasif, Kumbukumbu na Oysterbay ili kujenga tabia ya kujisomea kwa watoto tangu utotoni. Klabu ya Kujisomea ya Shule ya Msingi Oysterbay imezinduliwa rasmi jana tarehe 31 Julai 2013 kwa kukabidhiwa mashelfu na vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Soma Book Café pamoja na Book Aid International kupitia Maktaba Kuu ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...