Hapa ndipo ufunguzi wa movie utafanyika....wahi siti yako mapema kwani kila kitu kitakwenda kwa time. Ile movie iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi ndani na nje ya nchi sasa imekamilika..Njoo ushuhudie vijana wapya ambao wamejaribu kukuonyesha uwezo wa juu kisanii katika tasnia hii ya filamu.Haijawahi kutokea na usisubiri kuhadithiwa maana uhondo utauona mwenyewe siku ya jumamosi tarehe 31/08/2013 a ndani ya jiji la waungwana Den Haag nchini Uholanzi .Siku hii ni siku ya Ufunguzi ndio siku itakayoonyeshwa movie nzima ndani ya ukumbi wa Theater de Vaillant,ukumbi utakuwa wazi kuanzia saa kumi kamili jioni...tiketi zitauzwa hapohapo mlangoni kwa kiasi kidogo sana ambacho kila mmoja atakimudu ni euro 5 tu.Movie itaanza kuonyeshwa saa kumi na nusu hivyo ukichelewa utakosa uhondo wa wasanii wapya ambao wamekuja kivingine kabisa. Wahi siti yako mapema kwani haitaruhusiwa mtu kusimama akiwa anaangalia Utamu huu wa karne.Ukumbi kama unavyouona hapo juu pichani... Anuani ni kama ifuatavyo:-
Theater de Vaillant
Hobbema straat 120

2526kt,den haag
Holland. Angalia kautamu kadogo ka Movie nzima hapa chini..Yani ni balaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...