Bingwa wa dunia mara mbili bondia Frawcois Botha (White Buffalo) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu pambano kati ya Francis Cheka na Phill William. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF) Howard Golberg.

Rais wa Shirikisho la mchezo wa ngumi duniani (WBF) Howard Golberg akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo walipokuwa wanazungumzia pambano la mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phill William kutoka Marekani litakalofanyika tarehe jumamosi tarehehe 31 Agosti jijini Dar es Salaam.Pambano hilo limedhamini kwa ushirikiano baina ya kampuni za Hall of Fame na Nai Incoperation.
Rais wa chama cha ngumi Tanzania Yassin Abdalla akionyesha mkanda amboa utakuwa unashindaniwa katika pambano a ngumi baina ya Francis Cheka na Phill William, Pambano hilo litafanyika jumamosi katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waliosimama mbele kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Juliana Yasoda, Afisa Mkuu wa Kampuni ya Nai Incoperation Catherine Mateli,Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Nai Incoperation,Bingwa wa dunia mara mbili, bondia Frawcois Botha (White Buffalo),Bondia Phill William na Mratibu wa kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion wakiwa katika picha ya pamoja. Picha zote na Frank Shija - Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni kitu gani kimeeingiza TZ kwenye raMAni?

    Hapa wa TZ inapaswa kujiuliza. Kila mtu duniani anatamani kuja TZ. Bebu wenzangu nisaidie . Kuna nini TZ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...