Idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa wamekosea kujaza fomu zao za maombi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, wamejitokeza katika Ofisi za Makao Makuu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yaliyopo Barabara ya Sam Nujoma, eneo la Mwenge Dar Es Salaam ili kusahihisha makosa hayo.
Bodi ya Mikopo ilitoa muda wa siku kumi na nne (14), ambazo zinaisha tarehe 30 Agosti. 2013, kwa ajili ya wanafunzi ambao fomu zao za maombi ya Mikopo zilionekana kuwa na kasoro kwa kutosainiwa au kukosa viambatanishi muhimu ikiwa ni pamoja na nakala za vyeti vya kuzaliwa na vya taaluma.
Majina zaidi ya 6,000 ya waombaji Mikopo yenye dosari mbalimbali yamewekwa kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo ambayo ni www.heslb.go.tz ili kuwawezesha waombaji kugundua walichokosea na kuja Bodi au kutuma nyaraka husika kwenda Bodi,
Dosari mbalimbali kwenye fomu hizo za maombi ya Mikopo ni pamoja na kukosekana kwa sahihi za waombaji, kutobandikwa kwa picha za wadhamini, vyeti vya kuzaliwa na hata vyeti vya kuhitimu kidato cha nne kutoambatanishwa.
Umati wa wanafunzi ukiwa Umefurika kupata maelekezo ya kasoro zilizojitokeza kwenye fomu zao za maombi ya Mikopo kwa ajili ya Elimu ya Juu.
Mmoja wa waombaji mikopo ambaye hakuwa ameweka sahihi katika mkataba wake wa kuomba Mikopo akiweka sahihi mbele ya Ofisa wa Bodi ya Mikopo.
Ofisa wa Bodi ya Mikopo (kushoto) akiwaonyesha baadhi ya waombaji Mikopo kasoro zilizojitokeza katika fomu zao.
Mmoja wa waombaji wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu akikagua fomu yake ya maombi ya Mikopo kwa umakini katika Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Picha zote na Sunday Charles-Idara ya Habari, Elimu na Mawasiliano, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.


.png)
.png)
.png)
.png)
Kweli bongo tambalare! Tutatumia files na physical paper work mpaka lini ???
ReplyDeleteMdau wa kwanza kuhamia kwenye stage hiyo lazima kwanza matatizo muhimu yarekebishwe kama vile umeme na internet ya uhakika huwezi jaza form online wakati umeme haupo au ghafla unakatika au internet ya mashaka page moja inaload kwa dakika 10. Kwa hali ya sasa ni bora tutumie hivyo hivyo tuu makaratasi
ReplyDelete