Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO  Bw. Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa News for Rwanda na  wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.

“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Madai  hayo  yaliandikwa  jana  na  mitandao  ya  Rwanda  wakidai  kuwa  mama  Salma  Kikwete  ni  Mnyarwanda  na  ni  binamu  wa  aliyekuwa  rais  wa  zamani  wa  Rwanda. 
Wakati huo huo, wadadisi wa mambo wa kimataifa wameonesha kushangazwa na hatua ya makusidi ya Wanyarwanda ya kujaribu kumpakazia Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mmakonde  wa Lindi, kwa kumzushia mambo ya ajabu na kushangaa zaidi kuona mitandao hiyo ya udaku ya Rwanda haijaonesha jinsi Rais Kagame alivyovurumishiwa mawe na Wanyarwanda wenzake alipokuwa Chuo Kikuu ya Oxford nchini Uingereza.

"Unajua ustaarabu wa Watanzania ni wa hali ya juu ndio maana mitandao yake iliamua kuacha kuripoti habari za kutukanwa na kupigwa mawe Rais Kagame na Wanyarwanda wenzake wanaomchukia (angalia video) alipotembelea Chuo Kikuu cha Oxford hivi karibuni", amesema mdadisi mmoja  wa Uingereza, James Parker wa North London.

Mdadisi mwingine wa Uingereza, Bw. Mark Sutton, amesema hiyo ni moja ya njia chafu za Wanyarwanda katika kujaribu kulipiza kisasi kwa kutimuliwa maelfu ya ndugu zao waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania, na sasa wanahaha wapi kwa kuwaweka kwenye ka-nchi hako kadogo ka Afrika Mashariki.
"Kutimuliwa kwa Wanyarwanda nchini Tanzania kutaleta vituko vingi sana, na hii ya kumsingizia Mama Salma Kikwete kuwa anahusiana nao ni mojawapo - mengi yatakuja na Watanzania wasishangae maana Wanyarwanda wametaharuki na hawajui wafanyeje kwa kupokea zaidi ya wenzao 10,000 waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania," amesema mdadisi mwingine, Adam Hayes.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Kwa kweli nimeisoma habari jana kwenye ule mtandao wa Kinyarwanda kwa hasira sana nikatafakari nini cha kufanya kwa karibu, nikaona ngoja ni vite subira nione michuzi atakuja nayo vipi, nashkuru imezungumziwa. Kuongeza chumvi wanasema hata JK na Mkapa sio raia.

    http://www.newsofrwanda.com/breaking/20078/if-president-kikwete-is-tanzanian-then-most-rwandans-being-expelled-are-tanzanians-too/

    Ama kweli huku ni kutapatapa lakini hakupaswi kudharauliwa. Vita namba moja mbele yetu dhidi ya wanyarwanda ni kuchukua tahadhari kama taifa na kama mtu binafsi bila kukurupuka.

    sesophy

    ReplyDelete
  2. Damn, its like they are chasing a thief!are you sure this was a presidential trip?If yes then,something should be wrong.

    ReplyDelete
  3. Ukiachilia mbali mzozo uliopo, nilichokiona hapa ni nidhamu ya hali ya juu iliyooneshwa na polisi,ebu fikiria kama ingekua huko Tanzania kisiwa cha amani,nadhani damu ingemwagika sana kwa raia.

    ReplyDelete
  4. Unajua huyu Kagame visa vyake tumevisikia siku nyingi na kwa fikra zangu siku zake madarakani sasa zinahesabika.
    Yasemekana huyu ana mchango wake katika vurugu la Congo.
    Naamini viongozi wa nchi jirani naye wameshabaini hatari ya yeye kuendelea kuwepo madarakani na wanamtayarishia safari yake.
    Mshamba sana huyu!

    ReplyDelete
  5. Hapo sijaona polisi kufyatua bomu wala viongozi wa chadema kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi a.k.a. ugaidi. Hao polisi wamefundishwa jinsi ya kuthamini haki za binadamu.

    ReplyDelete
  6. Kelele za mpangaji hazimzuwii mwenye nyumba kupata usingizi...hao wanyarwanda wanatapatapa tuu lakini hakuna hata Mtz mmoja anaweza kuamini hizo story za kashfa kwa mh. rais wetu...muhimu ni wao waondoke banaa wakabanane huko huko kwao...hili zoezi naomba lisiishie huko Kagera,Kigoma na Geita bali lihamie na mijini pia...ili tuwasokomeze wote waende zao kwao bongo sio shamba la bibi...mh. rais tuko pamoja sana kwa hili...uzalendo kwanza vyama baadae!!
    Mdau wa UK.

    ReplyDelete
  7. Naunga mkono hoja ya kuwaondoa wanyarwanda wana dharau sana - hasa Watusi. Huwezi ukaenda kwa jirani kutafuta msaada halafu ukamdharau na msaada wake.

    ReplyDelete
  8. KAGAME nilikuwa namuheshimu sana, na alikuwa role model wangu, everytime nilikuwa namtumia kama mfano mzuri wa marais wa Africa ambao wapo strong na wana focus..Duh kumbe ovyoooo kama Babu Wenger, Nafikiri ndio maana pia anashabikia Arsenal,Lol! AMEJIVUNJIA HESHIMA. Na siku zake zimeisha tunamnyofoa soon pale, si unajua sisi ndio tuna control hii East Africa. Museveni mwenzake yupo kimyaa anakula Bata tu, kwutwa anatoa Ngao na Heshima kwa baba wa Taifa, mara misa za kumuombea Baba wa Taifa Mwl. J. Nyerere, anafikiri Museveni Fala? Kenya walichapana uchaguzi wa juzi tukaenda watuliza tukamweka Kibaki na Laila. Awaulize wenzie ndo atajua sisi ni akina nani, Sasa tunamwambia Adui muombee Njaa tu. Tunarudisha Watu wake wote kwao alafu tunafunga mipaka yetu na yeye tuone itakuwaje! Nchi yenyewe kama mkoa wa TANGA tu.

    ReplyDelete
  9. Jamani ni hatari sana kuwa na Rais kama huyu wa Rwannda. Sasa hakubaliki kwa wanyarwanda. Pia kumsingizia mama Salma Kikwete ni raia wa Rwanda nayo ni kali ya mwaka, au wanaona alivyo mzuri, mrembo na anavutia wameona hicho ndio kigezo waamue kusema ni wa kwao! Mungu ibariki Tz na wananchi wake.

    ReplyDelete
  10. Lakini mbona hawa wako wengi katika vyeo serikali. Hivi hawajulikani kwani. Halafu si wana umoja wao wa watu wanotoka katika mipaka ya Kagera, Kigoma na Tabora. Pale Chuo Kikuu walikuwa wanakuja kutoka hasa Kigoma na Tabora kijijini, wanafunzi akiulizwa cheti cha kuzaliwa ambao wamezaliwa miaka ya 70 wengi wao walikuwa hawana. Lakini wakienda RITA(Zamani ikiitwa.......) wanapata affidavit. Tatizo ni Serikali yenyewe sio wanyarwanda. Its too late now. Wengine wameshaowa na kuzaliana. Tena na Wabunge wapo ambao sasa wameshanaturalize. Nilipokuwa Uingereza nilisikia mmoja wa watoto wa mkubwa mmoja alijilipua msomali kwa sababu ana features za kisomali kama warwanda wengi walivyo.

    ReplyDelete
  11. Rais wetu jamani ni mwelewa sana yaani kapigilia mulemule!! YaaniKAGAME kamwaga mboga nasie Amiri JESHI WETU KAMWAGA UGALI, PATAMU HAPO.Dawa ya mtu mpumbavu sikubishana nae unaangalia tu wapi pa kumkomesha na matokeo yake ndo hayoo! KUNA PAMBIO LINASEMA ULIMI KIUNGO KIDOGO LAKINI MATATIZO YAKE NI MAKUBWA HAYA SASA KAGAME KULA FUPA HILOOO!

    ReplyDelete
  12. Rwanda wasitape tape kupakazia Uraia wa kwao Watanzania wanao heshimika kama Mama Salma Kikwete.

    Nimefurahishwa sana na Tamko la Mhe.Waziri wa Mambo ya Ndani Dr.Emmanuel Nchimbi ya kuwa URAIA WOWOTE ULE, HASA WA TANZANIA UNAPATIKANA KWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI HATA KAMA ULIZALIWA TANZANIA.

    HIVYO WANYARWANDA WANATAMBULIKA NA WATANZANIA WANATAMBULIKA WAZI.

    ___________________________________
    KIGEZO KIMOJAWAPO CHA URAIA WA MOJA KWA MOJA KUWA MTANZANIA NI
    ___________________________________
    NI KUWA ENDAPO WAZAZI WAKO WALIKUWEPO KTK NCHI YA TANGANYIKA KUTOKEA KABLA YA TAREHE 9 DESEMBA 1961 AMA ZANZIBAR KUTOKEA KABLA YA TAREHE 12 JANUARI 1964,

    :::::HAPO WEWE NI MTANZANIA KWA KUWA UTAKUWA UMEZALIWA NA WAZAZI WATANZANIA KWA KIGEZO:::::::

    ReplyDelete
  13. Eti nini?

    Mama Salma Kikwete ni Banyamulenge mwenzenu?

    TAFADHALI KAGAME NA WEWE TUTAKE RADHI!

    WANYARWANDA NA NINYI MTUOMBE RADHI WATANZANIA !!!

    NA WEWE TUOMBE RADHI KWA KAULI YAKO!

    WENGI MTAKUWA MNAKIJUA VIZURI KISWAHILI NA WENGI MLITUKUWA MNAISHI TANZANIA KINYUME CHA SHERIA, NASISITIZA MTUOMBE RADHI WATANZANIA UUNGWANA NI VITENDO!

    ReplyDelete
  14. Ha ha ha ha haha!

    Toka lini Mama Salma Kikwete akawa na Unasaba wa Rwanda?

    Kama madai yenu yana ukweli naomba mnipe malelezo zilipo Ofisi ya Ubalozi wa Rwanda hapa Dar na Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Kigali:

    MCHEZO WA MPIRA HUWA NA MZUNGOKO WA MECHI ZA NYUMBANI NA UGENINI:

    1.MECHI YA NYUMBANI(DAR ESA SALAAM-TANZANIA)
    NITAFIKA MPAKA HAPO NA KUNYA MCHANA KWEUPE BILA AIBU, ILI MRADI ASKARI WENU WASINITIMUE!

    2.MECHI YA UGENINI (KIGALI-RWANDA)
    MZUNGOKO WA MECHI RAUNDI YA PILI MECHI YA UGENINI NITAPANDA NDEGE HADI KIGALI NIKIFIKA NITAKUNYA MBELE YA UBALOZI WA TANZANIA MCHANA KWEUPE!

    ReplyDelete
  15. Mnhhh mtutake radhi WATANZANIA na ninyi RWANDA!

    Rwanda tafadhali tuheshimiane mtuondolee uchuro!

    Yaani First Lady wetu Mama Salma Kikwete naye Banyamulenge mwenzenu?

    ReplyDelete
  16. Hawa jamaa wanatapatapa, Dunia nzima hakuna nchi ambayo utaishi kiharamu then uachwe, ili iweje. Sasa kama si kuchanganyikiwa ni nini, toka lini mgeni akatuambia nani mtanzania nani siyo? Hii singo haijauza wakatafute nyingine, na hakuna itakayouza. Hawajui kwamba Diplomasia ya JK iko juu sana, Mungu amzidishie hekma. Yeye huwa ni mtulivu si mropokaji ila akiibuka; wenye akili watajua kwamba ameinuka. Bravo Mhe. Rais,waache waseme wee chapa kazi, watanzania tuko nyuma yako japo pia tunakuomba wasikilize hao waislamu hoja yao(ingilia kati) ili upendo miongoni mwa watanzania uimarike na Amani huko nyumbani itawale kama kawaida yetu. Kamwe dini isiwe kigezo cha kututenganisha na utanzania wetu.

    ReplyDelete
  17. Akuuu Rwanda tuacheni wana wa wenzenu Tanzania!

    Misisafirie nyota ya mwenzenu, tumesha watimua Tanzania Serikali yenu ipokee ugeni kama ilivvyoahidi bebeni mzigo wenu wenyewe msitushirikishe ktk utatuzi wa shida zenu.

    Tumesha wabeba sana miaka nenda miaka rudi sasa tumechoka !

    Limewakwama wenyewe !

    Mtaishi vipi ktk nchi yenu kiduchu?

    Mtaishi hadi juu ya mapaa ya nyumba?

    Mtaishi kuanzia uvunguni mwa vitanda vyenu hadi juu ya Madari ya nyumba zenu?

    Mtaishi hadi Milimani, mashambani na Misituni?


    Nchi yenu Rwanda ukubwa wake Ekari mbili wageni 10,000 wamewasili huku idadi mliopo huko 10 Milioni.

    Si Mtalijua Jiji???

    ReplyDelete
  18. Eh kweli kagame kamwaga mboga JK kamwaga ugali,wacha tuendelee kusikiliza,yatajitokeza mengi kuliko tunavyotarajia.

    ReplyDelete
  19. Ndugu zangu Watanzania lazma tuelewe kwamba yote hao Wanyarwanda wanazungumzia kuhusu Mh.Rais wetu ni propaganda,sababu Mh. Kikwete aliwaambia ukweli huko Ethiopia.
    Hii nchi jirani ni tishio la Amani Afrika Mashariki na Kati na hizi propaganda zao wamezisambaza hata Kongo kusema kwama Rais Joseph Kabila si raia wa Kongo.Kinacho shangaza hilo kabila lao sio wazawa wa Rwanda inajulikana wametokea huko juu Ethiopia. Tanzania ni Kisiwa cha Amani,hongera sana Ndugu Kikwete kwa wazo lako la busara kuwaambia lazma wakae na waasi wao ili amani idumu bara letu Afrika.

    ReplyDelete
  20. najisikia furaha sana kuona watanzania tunakua kitu kimoja linapotokea jambo kama hili.Mh Rais fanya mambo baba watanzania tunaona na tuko nyuma yako,

    ReplyDelete
  21. Katika ishu hii ya msafara wa Kagame kutupiwa mawe, mie mwenzenu nimeiangalia kimtazamo mwengine kabisa. Hivi kama hii tabia ya kuwatoa mbio viongozi wabadhirifu wa mali za umma wa kiafrika ikienea nje za nchi, si kutakuwa na mtizamo mwengine kabisa?

    ReplyDelete
  22. Mbona nasikia huko kwao kuzuri kupitiliza, nchi ya kuvutia ya vilima vingi, nchi ya maziwa na asali, barabara zinapigwa deki, air freshners kila kona, huoni hata kipande cha karatasi, nchi imepangiliwa, misifa kibao. Sasa kwa nini wanang'ang'ania huku kwetu? si warudi huko kwao wanokufananisha na bustani ya Eden?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...