Viongozi wakuu wa Wizara ya Maji, katikati ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, wapili kushoto, Naibu Waziri Dk. Binilith Mahenge, wapili kulia ni Katibu Mkuu Mhandisi Christopher Sayi, wakwanza kulia Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Bashiru Mrindoko na wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Neema Cornelio waliokaa nyuma yao ni wakurugenzi na wakuu wa Idara wa Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Christopher Sayi akiteta jambo na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe kabla ya kuanza kikao na wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akihutubia wafanyakazi wa Wizara ya Maji, katika kikao alichokiitisha yeye mwenyewe ili kuongea na wafanyakazi wote. Mkutano huo ulifanyika Makao makuu ya Wizara hiyo, Ubungo Maji.
Bi. Sara Masangi, akimuomba Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe juu ya kusaidiwa kupewa kazi katika kitengo chao cha Drilling and Dam Construction Agency (DDCA). Nyuma yake ni baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, akiwataka wafanyakzi wa Wizara hiyo kufanyakazi kwa bidii na kwa uwajibikaji ili kufikia lengo la kuwapatia majisafi na salama wananchi wote kwa kadri iwezekanavyo.
Huyu mkuu wa maji naona muda mwingi koti lake ni hilo tu? so analipenda zaidi ya yale mengine au?
ReplyDeleteJe tangu tuliposema tatizo la maji lingeishia 1990, hadi leo watu Tanzania bado tunaona kupata maji ni swala la starehe - luxury? Mungu ibariki nji yetu
ReplyDelete