Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudencia
Kabaka (Kulia) akijiandikisha kuwa mwanachama wa PPF kupitia Mfumo wa
Hiari (Mfumo wa Uwekezaji Amana). Pembeni yake ni Afisa Mwandamizi wa
PPF Kanda ya Ilala, Mordgard Lumbanga akifuatiwa na Meneja Uhusiano wa
Mfuko huo Lulu Mengele na Afisa Uendeshaji Kanda ya Ilala, Iddi Kibire.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia
Kabaka (Kulia) akipeana mkono na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni
wa PPF, Lulu Mengele mara baada ya kupokea kadi ya uanachama wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF. Wakati huo huo Msaidizi wa Waziri wa Kazi na Ajira,
Saimon Mwanajali naye alijiunga na Mfuko huo kama anavyoonekana katika
picha.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia
Kabaka (Kulia), akionyesha kwa furaha kadi ya uanachama wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, mara baada ya kujiunga rasmi na mfuko huo. Mwisho
kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele pamoja na Afisa
Uendeshaji Kanda ya Ilala, Iddi Kibire na Afisa Mwanadamizi wa Kanda
hiyo ya PPF, Mordagard Lumbanga wakifurahia tukio hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...