Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano  ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
 Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
 Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
 Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Prepare for watoto wenye asili ya kichina kuanza kuzaliwa maeneo yanapopita mabomba hayo!! Its all good, ahaaa!!

    ReplyDelete
  2. HONGERA MR MUHONGO KWA KAZI NZURI.HAYA NDIYO MAENDELEO.

    ReplyDelete
  3. Aibu kabisa, Kuona wafanyakazi wachini kabisa kutoka China wakija kufanya kazi Tanzania na Wazawa wanaachwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...