Rundo la takataka linalosemekana kumwagwa na gari la taka barabara ya Nyerere katika mataa ya kona ya Vingunguti jioni ya leo. Ripota wa zamu aliye katika doria ya sikukuu ya Iddi ambaye amefika hapo kiasi cha nusu saa iliyopita anasema gari hilo lilipata ajali sehemu hiyo na askari trafiki aliyefika kuhudumu aliamuru liende kituoni bila hizo takataka na ndipo likafanya hayo uyaonayo. Tunafuatilia swala hili la aibu na tutawajulisha matokeo yake
Magari yakipita kwa shida eneo hilo
Bado haiingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu kufanya haya
Nani wa kulaumiwa katika hili?
Cha kushangaza, tume ya jiji ipo, mkuu wa mkoa yupo, na wahusika wa jiji wapo...sasa nini kinashindikana? Tumsubiri rais mwingine wa Marekani aje baada ya miaka 4 ndipo tume ya jiji itafanya tena usafi. Kikwete unapochagua viongozi wazembe na wewe pia unaonekana mzembe. This is just too much now na ni haibu kwa taifaa.
ReplyDeleteHiyo ndo Bongo Daresalam .
ReplyDeleteJiji limefikia kuingia mkataba ma kampuni sijui YONO au MAJEMBE AUCTIONS eti kukamata watu walioegesha vibaya magari yao badala ya kuwacontract hawa kukamata wanaotupa taka hovyo(Naongelea vipaumbele).Wiki iliyopita nilibahatika kutembelea China(Ankal nitakutumia picha moja baadae ye mama lishe wa huko),wale jamaa ni wasafi,yaani ni wasafi.Uchafu upo lakini si kama huu wa Daresalaam,lakini kwa ujumla ni wasafi.JIJI la Daresalaam ni chafu,yaani ni chafu.Usafi unaanzia kwako nyumbani.Watu wengi Daresalaam tuwachafu na tunawafundisha watoto wetu UCHAFU hovyo.Lazima watotot hawa watakua hivyo hivyo
ReplyDeleteDavid V
Hii hali kweli nimeiona mwenyewe jana usiku wa saa tano, nimepita pale nikiwa kwenye gari nikaziona, hata kama gari ilipata ajali sii ingeletwa ingine ibebe hzo tako halafu ndo hili lingine liende kituoni, thnking capacity 0.
ReplyDeleteHaiwezekani aliyemwaga hizi taka ni mtanzania. Maana mtanzania anaipenda sana nchi yake. Hataki uchafu ambao utaleta maradhi kama malaria n.k. Kwa hio wale walio ona ushushaji wa huu mzigo wa toe ripoti discretely. And action ichukuliwe. Lets look after our Tanzania. Lets be proud of it. We the people is what MADE TZ beautiful and peaceful. But somehow we have been infilterated by aliens who are destroying us and we are just letting them. People seem demoralised. WHY? Someone has to be in a position to do or say something. Usafi wa Mazingira' day should be start.
ReplyDeleteAnkali peleka hii Guiness records tunaweza kuingia kwenye maajabu ya ulimwengu!
ReplyDeletesasa dereva wa gari la taka kashaiba mafuta, taa ya mafuta imemwakia Vingunguti akipiga hesabu dampo lipo mbali mpaka Pugu Kinyamwezi next anapiga jicho kushoto kulia hakuna soo binua tipa mwaga taka, anapiga u-turn yake pale kwenye taa huy anageuza zake mjini, mfukoni mambo mazuri ana hela yake ya kuuza mafuta ya wizi!
ReplyDeleteWewe mdau eti aliyemwaga radhi hapo kuwa si Mtanzania! Acha kujifariji na kuwatia wenzako ujinga: Ukweli wa mambo ni hivyo ndio tabia yetu halisia, ukiwa Dar jaribu tembelea Mbagala, Tegeta, Ilala, Buguruni.....halafu upime kauli yako.
ReplyDelete