Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel katika wiki ya usalama barabarani, mwandishi huyu alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini na India.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Airtel Tanzania ambao wamekuwa wadhamini wakuu wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa mwaka wa tano mfululizo Bi. Beatrice Singano Mallya akisalimiana na Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel katika wiki hii ya usalama barabarani mkoani mwanza. Athumani alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini na India.
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu ya Airtel imesema kuwa itahakikisha suala la Usalama barabarani linazingatiwa na jamii ya Watanzania ili kupunguza ajali za barabarani .
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Mallya kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani,yanayofanyika Jijini Mwanza.
Alisema kama wadau wa usalama barabarani,wamedhamini maadhimisho hayo ili kuwezesha jamii kupata elimu na uelewa kuhusu matumizi ya barabara,sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani katika kupunguza ajali nchini.
alisema ajali nyingi nchini zinachelewesha maendeleo na kupunguza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Sisi kama wadau tumedhamini maadhimisho haya kwa mwaka wa tano mfululizo,lengo letu tunataka jamii ipate uelewa na hatimaye kupunguza ajali za barabarani zinaoweza kuepukika,ndiyo sababu tuko hapa,”alisema.
Alisema kutokana na kuonesha umahiri wameanzisha mfumo mpya wa ulipiaji wa leseni za magari kwa kupitia njia ya Airtel Money.
Hivi huyu Mwandishi bado yupo TSN? maana kwa mazingira ya Kibongo na maono ya taasisi zetu wanaweza kama ni mzigo lakini kiuhalisia,anatakiwa afanyiwe" Special rehabilitation" aweze kufanya kazi hiyo hiyo ila kwa mazingira rafiki ya ulemavu wake.
ReplyDeleteNatamani kujua wamempangia kazi gani sasa,ni ukweli usiopingika kapata tiba ya kutosha ila kama ameachwa hivyo itabidi awe tegemezi ambapo bado anaweza kufanya kazi na kutoa mchango mkubwa katika taifa hili.
Hakika tunahitaji nguvu ya ziada kuhakikisha usalama katika barabara zetu Tanzania, hasa katika jiji la Dar es salaam, maana siku hizi zimegeuka uwanja wa ubabe, saa igine huwa najiuliza hivi nani anawapa leseni watu hawa? hata sheria za msingi tu hawajui wengi wao, watu wenye umri chini ya miaka 18 nao wako barabarani. Ni fujo tu.
ReplyDeleteJamani kweli kabla hujafa hujaumbika pole sana kaka yangu athumani historia yko inasikitisha sana ila jitahidi kutumia uwezo uliobaki nao hata kama mikono yako haifanyi kazi basi tumia akili yako na vinginevyo kutokana na mazingira yanayo kuzunguka na inshALLAH M/mungu akupe subira.
ReplyDelete