Na Dkt Noorali T. Jiwaji
Leo Jumapili tarehe 8 Septemba, upande wa magharibi karibu na upeo, utauona Mwezi ukiosogea nafasi yake angani mbele ya macho yako, ukiuangalia kwa saa moja hivi kuanzia baada tu ya machweo, hadi baada ya saa mbili hivi. (angalia picha chini)

Nyota ya Spika inayoonekana kushoto wa Mwezi mwandamo ipo juu kidogo tu ya Mwezi, lakini baada tu ya saa moja hivi utaona nyota ya Spika iko chini kidogo ya Mwezi mwandamo.

Kilichotokea kihalisi ni kwamba kwa vile Mwezi unatembea kwa kasi kubwa katika mzunguko wake wakati nyota hasizogei, kihalisi, ni Mwezi uliosogea kupanda juu.

Sayari zote, pamoja na Mwezi, husogea kutoka magharibi kwenda mashariki ukilinganisha na nyota, ambazo hazisogei angani kwa vile zipo mbali mno na sisi.

Nyota angavu sana inayoonekana juu ya Mwezi si nyingine ila 'nyota ya jioni' ambayo ni sayari ya Zuhura.  Mwezi mwandamo na nyota angavu ya Zuhura inatoa mandhari ya kuvutia sana angani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Napenda unajimu wako sio kama ule mwingine!

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...