Mjumbe Maalum  wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika  Kanda ya Maziwa Makuu,  Bi. Mary  Robinson
Na Mwandishi Maalum
Kufuatia  kurejea tena kwa  mapigano makali yaliyotokea wiki iliyopita kati ya majeshi  ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  ( FARD) yakisaidiwa na  Jeshi la MONUSCO  na kundi la   waasi  la M23. Umoja wa Mataifa sasa  unajaribu kutafuta suluhu ya kidiplomasia inayolenga katika kujaribu  kuweka sawa hali ya mambo.
 Mapingano  hayo ambayo  siyo tu  yanasadikiwa kuliondoa kundi la M23   katika ngome yake ya vilima vya  Kibati  Magharibi ya Kivu.   Yamelaaniwa vikali na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu  Ban ki  Moon hasa baada ya kundi hilo la M23 kusababisha  kifo cha  mwanajeshi Mtanzania na kujeruhi wengine kumi wakiwamo wanajeshi  kutoka Afrika ya Kusini.
 Mchakato huo wa   kisiasa  unafanywa  na Mjumbe Maalum  wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika  Kanda ya Maziwa Makuu,  Bi. Mary  Robinson, ambaye amewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya  jumapili na kutoa  rambirambi zake kwa wahanga wa  mapigano hayo.
Taarifa kutoka  ofisi ya  Mjumbe huyo Maalum, inataarifu kwamba, Katika  mchakato huo wa kutafuta suluhu ya  kidiplomasia ,  Mary  Robinson ataongoza ujumbe  maalum utakaowahusisha  Mwakilishi wa  Umoja wa Afrika,  Bw. Boubacar Diaraa,  Bw. Russ Feigold, ambaye ni Mjumbe  Maalum wa Serikali ya  Marekani katika Eneo la  Maziwa Makuu, Bw. Martin Kobler Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu  katika DRC na  Mkuu wa MONUSCO, wakati Jumuiya ya Ulaya itawakilishwa na  Mratibu Mwandamizi katika Maziwa Makuu,  Bw. Koen Vervaeke.
Kabla ya kuungana na ujumbe huo, Bi. Mary Robison atafanya mazungumzo  ya ndani na washirika wa Umoja wa Mataifa katika DRC na kisha atakwenda Goma  kama hatua ya kuonyesha mshikamano wake na  wananchi wa eneo hilo na  Jeshi la Kulinda  Amani  la Umoja wa Mataifa  ( MONUSCO).
Kwa mujibu wa Ofisi ya   Bi Mary Robison    ziara ya Mjumbe huyo na ujumbe wake,   pamoja na kutembelea DRC pia watakwenda  Uganda na Rwanda   kati ya  Septemba 4-7, ambapo  pamoja na mambo mengine  watakutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa na Mashirika ya Kiraia  pamoja  na kuhudhuriwa  kikao cha  dharura  cha Mkutano wa Kimataifa wa   Kanda ya Maziwa Makuu  ( IGCLR).
Taarifa hiyo inabainisha kwamba akiwa katika nchi hizo, Bi. Mary Robinson atasisitiza haja na umuhimu wa pande zinazohusika kusitisha vitendo vya  uhasama na kuelekeza nguvu  zao katika majadiliano ya kisasa  pamoja na mchakato wa Kampala  ( Kampala Process).
Aidha  inaelezwa  kwamba wakati Bi. Robison na ujumbe wake watakapohudhuria mkutano wa  IGCLR   utakaofanyika  Septemba   5 jijini Kampala,  watahimiza uharaka wa utekelezaji wa  Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama na maendeleo katika DRC na Eneo la Maziwa Makuu,  mpango ambao ulisainiwa mapema mwaka huu  na  nchi 11 na wadhamini  wanne wa kimataifa .
Ziara hiyo  ya Bi. Mary Robison na ujumbe wake inafuatia  kurejea upya kwa mapigano makali katika eneo la  Mashariki ya DRC   mapigano ambayo yameifanya  hali  ya mambo katika eneo la Maziwa  Mkuu kuwa tete, huku  kukiwa na ongezeko kubwa la wakimbizi, hali inayochagiza uharaka wa  kutafuta suluhu ya kisiasa ili kurejesha hali ya  utengamano katika  DRC na eneo la Maziwa Makuu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. M23 wajanja hao. wana-buy time ili wajikusanye nguvu na pia ili waweke maswala sawa na Washikaji zao Rwanda halafu wanawasha moto tena.
    Ningekuwa mie ningeendeleza kibano tu ili wasiwe hata na dakika ya kujisaidia hata haja ndogo hadi wamesambaratishwa au kutokomezwa kabisa. Hilo ndo lingekuwa fundisho kwa makundi mengine hasi. Lakini kwa mtindo huu ngoma itaibuka tu upya tena. Haya endeleeni kupumbazwa!!!!!

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa! taarifa haioneshi iwapo atakutana na wawakilishi wa M23 katika kuitafuta hiyo suluhu au kwa kuzitembelea nchi zilizotajwa ktk habari hii yatosha?

    ReplyDelete
  3. WE ANNOY WA KWANZA KAMA INGEKUWA WEWE SASA UNASUBIRI NINI SI UENDE TU UKAPIGANE KAMA VITA NI VIZURI?

    ReplyDelete
  4. hii vita haitakiwi kuisha ndugu .... wakubwa wa madini watakula (wataiba) wapi

    ReplyDelete
  5. UN na UNSC (UN SECURITY COUNCIL) mnachelewa nini?

    Mama Mary Robinson Rambirambi peke yake zitatufariji vipi Watanzania ambao kwa uchungu na masikitiko makubwa tunauliwa Majeshi yetu kwa kutetea ustawi wa Amani ya watu wengine wajinga na wasio na akili?

    Raisi Kagame ni nani katika dunia?

    Ina maana maslahi ya Kagame, Rwanda na M-23 ndio yawa gharimu watu maisha na tabu za bure?

    Kwa nini hadi sasa UN na Marekania yenye Nguvu za Kijeshi kama Dume la Simba wasitume ''DRONES'' (Madege yasoyo na Marubani na ya Kipelelezi) ili kumuumbua Kagame na Kundi lake M-23?

    ReplyDelete
  6. Jamani hili suala linaonekana ni la muhimu sana. Ninaomba jumuiya ya kimataifa iingilie. Ninawaonea sana huruma watu wa DRC...jamani hawa watu wanaoishi kwenye utajiri mwingi watakufa hadi lini? Ni Afrika gani? Jamani waafrika tuache kuwatesa waafrika wenzetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...