MCHUNGAJI Ambilikile Mwaisapila wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonyesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na baadaye kioo cha dunia.

Ametoa kauli hiyo jana asubuhi (Jumanne, Septemba 24, 2013) mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.

Mchungaji Mstaafu Mwaisapila maarufu kama Babu wa Samunge alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge. “Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. This guy has got blood on his hands, some stupid people believed his nonsense "kikombe" and as a result they day, he must be charged of false misrepresentation and fraud, but again some drs, prominent lawyers and top politician queued to have their share of the medically useless drink.

    ReplyDelete
  2. Wallah! huyu babu anataka tena kututapeli! Nami natabiri kuwa endapo atakuja na 'MUUJIZA' mwingine wa kitapeli ndio utakuwa mwisho wake namhakikishia!

    ReplyDelete
  3. mhhhh babu yesu atatua bongo akitokea mbinguni duuuu babu hii kali

    ReplyDelete
  4. Msiwe na Haraka Kumhukumu Mzee huyu. Mungu anatenda mambo yake kwa namna Binadamu hatujui kutokana na dhambi zetu na upeo wetu finyu na wa Kidunia.

    Mambo makubwa na watu maarufu wametokana na familia na taifa dogo na maskini. Na wakaleta mabadiliko makubwa mazuri ulimwenguni. Msikilize Mzee huyu; omba Mungu akufunulie na wewe upate kutambua ukweli wa tabihu zake. Chukua uamuzi kwa matashi yako. Sababu hata unachutuambia wewe, tunatia mashaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...