Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Dinka ya Uholanzi baada ya kuchangisha milioni themanini za ujenzi wa shule ya Dinka inayojengwa Arusha.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya DART ya Uholanzi baada ya kuzindua taasisi hiyo inayotafuta misaada ya kusaidia vijana Tanzania. Taasisi hiyo inasimamia na kuendesha kituo cha kusaidia vijana, Mwanza. Balozi Kamala amewashukuru Viongozi hao na amewaomba Watanzania wanaokaa katika nchi za Benelux kuchangamkia fursa mbalimbali zinzopatikana katika nchi za Benelux kusaidia nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safi sana kuona watanzania waliopo nje wanasaidia nchi yetu. Nimependezwa sana na hao wamama wa Uholanzi na juhudi zao wanazozifanya. Mungu awabariki sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...