Mwenyekiti wa muda wa TAWUTA Bw.Johansern B.Lwekamwa akionyesha cheti cha usajili wa chama cha TAWUTA, kushoto katika picha anaonekana Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Bibi Dorothy Uiso, pamoja na Ofisa wa Ofisi ya Msajili Bibi Lilian Muchuruza mwanzoni kulia.

Ofisi ya msajili wa Vyama vya wafanyakazi na Waajiri nchini iliyopo Wizara ya Kazi na Ajira imesajili rasmi chama cha wafanyakazi wa reli ya Tazara (TAWUTA) Tazara Workers Union-Tanzania tarehe 20/09/2013.

Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti cha usajili Bibi Dorothy Uiso, Msajili wa Vyama vya wafanyakazi na Waajiri alisema ‘madhumuni ya kusajili chama hicho ni kukipatia fursa ya kwenda kusimamia maslahi ya wafanyakazi wa reli ya Tazara pamoja na wanachama wa mamlaka hiyo’.

Bi D.Uiso alimkabidhi Bw.Johansern B.Lwekamwa ambaye ni mwenyekiti wa muda wa chama hicho cheti cha usajili kama ishara kuwa, chama kipo huru kuanza kufanya kazi zake bila pingamizi yoyote.

Ofisi za TAWUTA kwa sasa zipo Kiwalani jijini Dar es Salaam na zitaendesha shughuli zote za wanachama kwenye eneo hilo kwa muda hadi watakapopata eneo la kudumu.

Bibi Uiso alisistiza kuwa, wamekipa chama hiki usajili baada ya kutembelea eneo lao la kufanyia kazi na kuridhika na mazingira ya ofisi hiyo na kuwa yanafaa kufanyia shughuli zao zote za chama bila tatizo.

IMETOLEWA.

MS CONSOLATHA SHOO
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA KAZI NA AJIRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...