Na Dixon Busagaga, Moshi 
 HALI ya wasiwasi imetanda kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kujifanya ni daktari wa watoto akiwa kwenye wodi ya upasuaji. 
 Daktari huyo feki aliyefahamika kwa jina la , Alex Sumni Massawe alikamatwa jana majira ya saa 5 asubuhi na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia baada ya kukutana na mmoja wa wagonjwa ambaye alimuahidi kumfanyia mwanae wa kiume upasuaji wa ngozi. 
 Kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana aliyekuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji, Pamvelina Shirima alikutana na daktari huyo katika baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street (jina limehifadhiwa) na kumtoza sh.200,000 akidai zitatumika kuharakisha mwanae afanyiwe vipimo vya upasuaji. 
 Alex anadaiwa alitaka kumfanyia upasuaji kijana, Makasi Tipesa, mkazi wa Manispaa ya Moshi ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa muda mrefu sasa. 
 Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC, Bw. Gabriel Chisseo alisema daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali ya KCMC kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambaye amekuwa akijinasibu kwamba anafanya huduma hiyo kutokana na wito alionao katika fani hiyo.
 “Leo asubuhi(jana) mteja wetu ambaye amekuwa akitibiwa hapa alitapeliwa na huyu Alex , tulimkamata akiwa wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi cha sh.200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanae afanyiwe upasuaji wa ngozi", alisema Chisseo.
 Uongozi wa Hospitali ya KCMC umethibitisha kwamba mtu huyo aliyekamatwa ndani ya Hospitali hiyo, si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala kitambulisho kinachomtambulisha kitengo chake cha kazi. 
 Hivi karibu kumeibuka matukio ya watu kadhaa kujivika kuwa na taaluma mbalimbali ambazo si za kweli huku jeshi la polisi likifanikiwa kuwakamata wengine wakijifanya kuwa ni maofisa wa jeshi hilo ,wengine usalama wa taifa huku wengine wakijifanya asakri wa kikosi cha usalama barabarani.
 Afisa uhusiano wa hosptali ya Rufaa ya KCMC,Gabriel Chisseo akimwonesha anayedaiwa kujifanya daktari katika hosptali hiyo (Daktari Feki) aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe.
 Aliyejidai kuwa ni Daktari katika hosptali ya KCMC(Daktari Feki) aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo.
 Daktari Feki Masawe akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'.
 Daktari feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. UGUMU WA MAISHA KIPIMO CHA AKILI!

    Lakini siyo kwenye Fani nyeti kama Udakitari, angalau jamaa Alex angejiita hata Profesa lakini awe wa Dirisha la Pili la USAJILI YAANI PROFESA WA TIBA ASILIA (Mganga wa Kienyeji) ISINGEKUWA TATIZO SAANA MAANA HATA SERIKALI INATAMBUA WATAALAMU HAWA !

    Lakini Udakitari wa Magwanda Meupe ohhh hapana!,,,ndio maana Alex amejikuta chini ya mkono wa Dola.

    ReplyDelete
  2. Duhhh,

    Watanzania tuna Elimu za Kuzaliwa, ndio maana Alex amebeba Mkasi na kisu huko KCMC kutaka kufanya Upasuaji !!!

    ReplyDelete
  3. Hii Kasi ya maisha kazi tunayo!

    Udakitari?

    ReplyDelete
  4. kama unapenda utabibu vyuo mbona vipo vingi tu nchini na duniani.

    ReplyDelete
  5. Alex S. Massawe, Sinema umeicheza!

    Kutoka Maskani Mtaani hadi Wodini Hospitalini Kisu na Mkasi mikononi?

    Kweli umejiamini!

    Isipokuwa umekosea kidogo saana, makosa yako ni haya hapa ktk Sanaa yako:

    1.Jina ulilochagua ALEX MASSAWE ni baya kwa sababu yupo mkubwa wako ambaye hadi sasa anawakiwa na moto chini ya 'Wazee' Interpol akiwa Dubai Arabuni hivyo hilo jina lako limegonga vichwa vya 'Wazee' kwa haraka!

    2.Angalau ungevaa na Koti jeupe,
    3.Unge pachika pia Kipima Kasi ya Moyo Shingoni,

    4.Ungevaa Gloves nyeupe mikononi,
    5.Unge pachika Kipima joto kwenye mfuko wa juu wa Koti Jeupe.

    Kwa hayo Matano (5) unge yaweka ktk Sanaa ya Sinema yako hatari uliyo icheza Alex usinge bumbulukiwa kabisa, ungekuwa bado una endelea kuwapiga Mikasi na Visu vya Upasuaji Wagonjwa hapo KCMC !!!

    ReplyDelete
  6. Very sad!!!! Tamaa inapozidi utu. Majuzi ilikuwa trafiki feki, leo daktari feki, kesho ndege itarushwa na pilot feki. Safi sana kwa kuondowa huyu muuaji miongoni mwetu

    ReplyDelete
  7. Dr. Feki,

    Ungetumia akili kama Dakitari wa kweli kuyafikia malengo ya kimaisha kwa njia sahihi yote haya yasinge kukuta.

    Badala ya kutarajia Chips Kuku Mtaani kushushia kwa Bia baridi kwa mavuno ya Laki mbili Laki mbili ulizokuwa unawapiga watu na sasa unaelekea Lupango kupiga Dona kwa Maharage na kulala saa 12:00 Jioni!

    Ahhh, Dunia ngumu hivi?

    ReplyDelete
  8. Hakuna Wagonjwa mlio fanyiwa Upasuaji na Kishoka huyu?

    Kazi kwenu ombeni Msaada Serikalini mfanyiwe Uchunguzi!!!

    ReplyDelete
  9. Acheni maigizo bwana, hivi mazingira ya vyumba vya upasuaji vimekua rahisi namna hiyo kiasi cha mtu kufanya utapeli wa namna hii!

    ReplyDelete
  10. Dakitari Feki kingine kilicho kuponza ukakamatika kirahisi,

    Ni kuwa umevaa mawani ya Jua na ya kuchezea Dansi Klabu za usiku yenye vioo vyeusi badala ya mawani yenye vioo vyeupe ya Kisomi !!!

    Nani asiyejua ya kuwa Masomo ya Udakitari ni magumu na yanachukua muda mrefu hadi kuwauwa macho Wahitimu wa Udakitari?

    ReplyDelete
  11. Dr. wa kubabaisha huyu siyo bure!

    Pana uwezekano alikulwa anakula na mtu ambaye ni Mfanyakazi halali wa hapo.

    Inakuwa ni hivi, huyo mtu Mfanyakazi halali inawezekana hana ujuzi wa Kiusanii ndio maana akamtafuta ''JEMBE'' huyu Alex Mkata Vimeo bila Ganzi kutoka Maskani Mtaani ili apige kazi.

    Alex akibinywa ni lazima atamtaja na mtashangaa pana uwezekano atakuwa ni Stafu halali wa hapo KCMC!!

    Ama kama sio Stafu halali anaweza kuwa labda hata ni Muuza Vocha ama Mkata Manyasi, au Mfagizi wa maeneo hayo ya KCMC anaye pahafamu vizuri hapo na nyendo zake.

    Hivyo alipokuwa anakusanya fedha Shs. 200,000/= kwa kila kazi alikuwa anagawana na mwenzake!!!

    Bongo ndivyo tuijuavyo watu wanakula kwa Staili ya Mchezo wa Genge la Karata Tatu!

    ReplyDelete
  12. Tusishangae siku tukaja kuwa na Rais feki

    ReplyDelete
  13. Ohoooo,

    Jamani wooote mlio pigwa Visu na Mikasi na Kijogoo huyu mjiorodheshe tutembeze Bakuli mchangiwe Fedha ili mkafanyiwe Uchunguzi India!!!

    Ni vile jamaa hakuwa Dakitari bali alikuwa ni Mjasiriamali.

    ReplyDelete
  14. HII KCMC INATAKIWA IFUNGWE HADI UCHUNGUZI UKAMILIKE HUYU MTU ALIAJIRIWA NA NANI? UONGOZI UMETUMIKA KUFANYA UZEMBE HADI MTU HUYU KURUHUSIWA KUFANYA KAZI YA UDAKTARI. KAMA UONGOZI HUO ULIGUNDUA HUYU MTU NI FEKI, KWANINI KUMUWEKEA MTEGO WA POLISI? ANDEWEZA KUKATWA HATA AKIWA NYUMBANI KWAKE. KCMC INATAKIWA KUWALIPA FIDIA WAGONJWA WOTE WALIOHUDUMIWA NA HUYO TAPELE NA KUFUKUZA UONGOZI WOTE WA JUU. AFYA ZA WATU SIYO KITU CHA KUFANYIA MCHEZO.

    ReplyDelete
  15. mimi naona wamuajiri tu huyu muungwana katika wodi ya vichaa uhaba wa madaktari hapa kwetu ndio uliosababisha yote haya.
    madaktari wote wamekimbilia Botswana sasa sisi nani atatutibu.
    na kamchezo ka kukutana na madaktari sehemu za ulevi pia iwe mwiko huko kuna marubani feki na wahandisi bandia pia kwani mtu akishalewa unategemea akwambie hana kazi?
    mdau.
    moshi.

    ReplyDelete
  16. Tanzania kazi tunayo kwa upungufu wa Madakitari!

    Ndio maana utakuta hata mtu akiwa mgawa dawa Hospitalini ili mradi anafanya kazi Hospitali atajiita Dakitari!!!

    ReplyDelete
  17. Kama Madau wa Kwanza anavyosema,

    Usingejiweka katika Udakitari wa Magwanda meupe.

    Nchi nyingi kama kwa Mzee Mandela huko Kusini kwa kuwa inajulikana Tiba asilia ni kipaji cha Watanzania, hisomewi ni kukabidhiwa Mkoba badala la Udakitari wa (Koti Jeupe) ungechagua Tiba asilia ungevaa ngozi ya mbuzi kiunoni ama shuka Jeusi(Kaniki) !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...