
Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga akijaribu kuendesha gari walilopewa na Wizara ya Afya naUstawi wa Jamii jijini Dares Salaam.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya wa pili (kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watu wakati hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya Sh. milioni 38 jijini Dares Salaam
Picha zote na Magreth Kinabo –MAELEZO

Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga(aliyesimama) akiishukuru Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa msaada wa gari hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Crispin Meelana kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya.
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu),
Profesa Mark Mwandosya amesema Tanzania itafikia maendeleo ya hali ya juu
ifikapo mwaka 2025 hadi mwaka 2030 ikiwa watu watafanyakazi kwa upendo,
uzalendo na kujiamini.
Aidha Profesa Mwandosya amesema kwamba Serikali inajitahidi kufikisha
huduma zake kwa karibu na wananchi, licha ya kuwepo kwa changamoto za
kielimu na miundombinu, lakini mambo mengi yanafanyika,hivyo wenye macho
wanaona.
Kauli hiyo imetolewa na Profesa Mwandosya wakati hafla fupi
ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya
huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya
Sh. milioni 38 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam.
“ Mimi nina matumaini makubwa na nchi yetu ifikapo mwaka 2025 hadi
2030 tutakuwa ni nchi yenye watu wenye kipato cha kati.Pia ifikapo mwaka 2050
nchi yetu itakuwa imeendelea hakutakuwa na mtu mwenye kipato cha kati wala cha
chini kama ilivyo nchi ya Singapore,” alisema Profesa Mwandosya.
Profesa Mwandosya aliongeza kuwa gari hilo ni moja ya juhudi za
Serikali za kuhakikisha kuwa huduma zake zinaifikia jamii kila
mahali hususan kwenye maeneo ya vijijini.
“Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake mfano katika sekta ya elimu
kuna mambo mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika ikiwemo katika sekta
nyingi kama vile kwenye nishati gesi tunakwenda vizuri.
Tukisimamia vizuri rasilimali zetu ,basi hata huduma
tutazifikisha vizuri kwa wananchi,” alisisitiza.
“ Kila mtu duniani anasema Tanzania inapiga kasi katika
kuwaletea maendeleo wananchi . Mimi nadhani hatutarudi nyuma. Wale
wanaopiga kelele hautajafanya kitu ,lakini mwenye macho wanaona,” alisisitiza
Profesa Mwandosya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Charles Pallangyo
akizungumzia kuhusu gari hilo alisema litasaidia kuhimarisha huduma za chanjo
katika halimashauri hiyo na kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito na
watotowenye umri wa chini ya miaka mitano ili kutimiza malengo ya millinea ya
namba 4na 5 ifikapo mwaka 2015.
Naye Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando alisema nchi hivi
sasa imefikia wastani wa asilimia 92 katika huduma za chanjo kutoka asilimia 90
ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga aliishukuru wizara
hiyo kwa msaada huo ,ambapo alisema gari hilo litatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa ili kuinua kiwango cha huduma hiyo kwenye eneo hilo.
ya Rungwe Dk. Gilibert Tarimo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...