Mrembo Megan Young kutoka nchini Philippino,leo afanikiwa kunyakua Taji la Mrembo wa Dunia (Miss World 2013) katika onyesho kubwa lililomalizika hivi punde huko nchini Indonesia.Mshindi wa Pili katika Taji hilo ni Marine Lorphelin kutoka nchini Ufaransa na watatu ni Kutoka nchini Ghana,Carranzar NaaOkailey Shooter.
 Akisalimia mara tu baada ya kutangazwa mshindi.
Shangwe kwa pamoja.
 Mratibu wa mashindano ya Redd's Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa tatu kulia) akiwa na wadau wa masuala ya urembo, wakishuhudia live kupitia kwenye luninga  kilele cha mashindano ya Miss  World 2013 jioni hii kwenye mgahawa wa City Sports & Lounge, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwandaaji wa Redd's Miss Temeke, Benny Kisaka, Mr University 2002, Chuma Matokeo na kutoka kushoto ni Mratibu wa Uhusiano wa mashindano hayo, Innocent Melleck na Albert Makoye ambaye ni Mkuu wa Itifaki wa mashindano hayo.
 Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa (katikati) akiwa na warembo Glads Shao (kulia) na Latifa Mohamed, wakishuhudia mpambano huo wa Miss World uliokuwa unafanyika nchini Indonesia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hakika anastahili kuvikwa taji. Tz tujipange zaidi. Hongera miss wetu kwa nafasi uliyopata si haba though!

    ReplyDelete
  2. Mashindano yalikuwa mazuri sana na mamiss wote walipendeza sana,bongo bado majanga tujipange sana tu

    ReplyDelete
  3. hata huyu muandaaji pia kapitwa na wakati,jinsi dunia ilivyo sasa ijipime tu.tatizo umaskini umikithiri sana .jinsi alivyo hapo juu ,ni muda wake kuacha sasa ,lakini du kuacha kuandaa akiambiwa itakuwa vita kubwa ya ajabu.au mtajimbika ???????????????

    ReplyDelete
  4. I have a lot about them: Miss World, Miss East Africa, Miss Temeke - what do they actually do?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...