Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akionyesha ngao aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa bodi wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi URA-SACCOS, Naibu Kamishna wa Polisi, Thobias Andengenye. Ngao hiyo alikabidhiwa jana kama ishara ya IGP kuwa balozi wa saccos hiyo katika viwanja vya kilwa road wakati wa uzinduzi wa Tawi la URA-SACCOS la Kilwa Road.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Kilwa Road la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi URA-Saccos jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Saidi Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bahati nasibu ya kushindania pikipiki na cherehani itakayochezeshwa na Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, Ura Saccos tawi la kilwa road. Tawi hilo lilizinduliwa na IGP.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini , IGP Saidi Mwema akipasha na maofisa, wakaguzi na askari wa Jeshi la Polisi, wakati wa uzinduzi wa Tawi la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi Kilwa Road, Ura-Saccos jana jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi, Advera Senso akionyesha ngao aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa bodi ya Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, URA-SACCOSS. Ngao hiyo ni ishara ya kuwa balozi wa SACCOS hiyo ambayo tawi lake la Kilwa Road lilizinduliwa jana na IGP.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Jeshi la Polisi wakionyesha mahadhi ya makhirikhiri jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tawi la Kilwa Road la Chama cha kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, URA-SACCOS. (Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi).
Polisi Saccos?
ReplyDeleteDuhhh Polisi nayo ina Saccos?, kwa sasa hakuna atakaye kataa kuwa Polisi maana kuna Utajiri wa Mapesa!!!
Polisi muitimie vyema Saccos yenu, sio aje Mwanachama wa Saccos ambaye ni Bosi wa ;Polisi akope na siku ya kudaiwa atoe amri Kopulo Kibereriti nenda Kilwa Road URA-SACCOS kawaambie ''aroooo mimi Inspekita Marwa natoa amuri kamata yure Karani wa Madeni pale Polisi Saccos niretee Kituoni''
ReplyDeletePolisi angalau mtapunguza kula Rushwa !
ReplyDeleteMaana mfereji wa fedha za halali kupitia Saccos yenu mmesha upata kwa kuwa na URA-SACCOS.