Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani. 
Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda. 
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili. 
Viongozi hao wawili wako nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu – “International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR)” unaofanyika leo Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort. 
Viongozi wengine ambao wanahudhuria Mkutano huo ni pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR na mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU). 
Rais Kikwete na ujumbe wake amewasili Kampala asubuhi ya leo akitokea mjini Dodoma ambako aliwasili jana jioni kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu watatu na Naibu Makatibu Wakuuu wawili iliyofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma. 
 Rais Kikwete aliwasili Dodoma akitokea Mwanza ambako alihudhuria mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Dkt. Moses Samwel Kulola yaliyofanyika kwenye Kanisa la Bugando Calvary Temple, mjini Mwanza. 
 Imetolewa na;
 Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu, 
DAR ES SALAAM. 
 05 Septemba, 2013
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana faragha sambamba na mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala,Uganda, leo
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika mazungumzo na Marais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto), Rais Salva Kiir wa Sudan ya kusini na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda 
 Baadhi ya viongozi wan chi za jumuiya ya Maziwa Makuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi hizo uliofanyika jijini Kampala Uganda leo.Kutoka kushoto ni Rais Salva Kiir wa Sudani ya Kusini,Rais Joseph Kabila wa DRC,Rais Dkt.Jakaya Kikwete,Rais Yoweri Museveni wa Uganda,Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt.Nkosazana Dlamini Zuma na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda.Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Chonde chonde ndugu zangu tusimwamini tena huyo PK,hivi kwanini tusifanye mambo yetu ya ndani kwa umakini wahali ya juu kabisa PORT ya bagamoyo ianze mara moja na ujenzi wa njia mpya na za kisasa ambazo ziwe za kimataifa,sambamba na PORT ya Mtwara ijengwe upya na yenye kiwango cha juu tukumbuke Msumbiji uchumi wao unakuja juu sn ninjia nzuli kwetu na wao pia,Tanga PORT pia ijengwe upya Lindi pia PORT ijengwe mpya Jamani Uchumi tunao lakini tunaukalia ,Mijiges ndio hiyo na mijifuta ya kumwaga sasa tatizo nn hapa? 2015 tumpe kula ndugu MWAKIYEMBE ili awe Raisi wetu na Wazili Mkuu apewe DR Slaa tufike sehemu tuwacheni uvyama ili tulete maendeleo endelevu ndugu zanguni,wazili wa Mambo ya Ndani apewe Samweli Sita,wa Elimu Magufuli,Zito kabwe wa fedha,naapa hakiyamungu wala wasengetusumbua hao Majirani Mchwala,naitwa mdudu Kakakuona mwenye macho ma3,nanyie nisaidieni majina ya mawazili walio kosekana hapo angalizo wadau mchague majina ya wenye sifa za kuchapa kazi sio wale dolodolo coz hii ni kalne ya 21,mungu ibariki TZ na watu wake woooote,

    ReplyDelete
  2. JK be careful sana watu wa Region hiyo si wazuri sana kwa ufupi wana vinyongo thats their Nature na wanajiona kama wako special.fuatilia sherehe ya PK akikutana na watu wake Canada wanasema kabisa kuwa wana kitu so special so ni kwenda nao kwa akili sana ingawa tuna undugu wa damu Inteligence Tanzania must be seriouse kwani tuna maadui wengi sasa.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza umenena,lakini siungi mkono Slaa kuwa pm,ila wazo la kuchagua viongozi toka upinzani kufanya cabinet ya mseto kama znz naunga mkono. Zitto namkubali,lissu awe mwanasheria mkuu,na wa ccm,kina SAS,SITTA,MWAKYEMBE,MAGUFULI,TIBAIJUKA,WAPEWE,wengine kama mbowe na slaa walee chama chao,hatuwataki wanavurugu. Leteni majina mengine basi,

    ReplyDelete
  4. Mnajua waTZ kuishi vema na majirani ni vizuri sana , ila akili kichwani.


    Walichokifanya PK na JK ni kizuri sana. Wahenga walisema , fahari wawili wakigombana ziumiazo ni nyika.

    Kwa vile sasa wameelezana wakaelewana safi sana lakini akili kichwani

    ReplyDelete
  5. Rais Kikwete ni Mwanadiplomasia aliyebobea. Anajua fika ni nini kinachoendelea na nina imani kuwa hawezi kurubuniwa na tabasamu au unafiki wa aina yoyote. Wa TZ tupo pamoja nawe Rais Wetu Mpendwa

    ReplyDelete
  6. Body language tells all. Picha ya kwanza inaonyesha JK is all about mending the broken relationship.. Akiwa amepiga hatua kubwa, kanyoosha mkono wake with a big smile. Mwenzake Kagame hatua yake aliyopiga ni kama ya kujilazimisha na inaonyesha kabisa alikuwa anasubiri JK amsogelee, smile yake haiko real, to me he seems to be all fake.. Watanzania we have to take the mending of relationship with this neighbour of ours with a grain of salt..as it may not be at all what it seems to be..

    ReplyDelete
  7. Raisi Kikwete hana wasiwasi amewafunika vibaya sana hao akina K3 na Vikao vyao vya Miundo mbinu Mombasa walivyo mtenga kuhudhuria.

    Wengi hamfuatilii mambo yanavyokwenda angalieni hapo chini.

    Ni kuwa,

    -Wao K3 (Kenyatta, Kaguta na Kagame) na Mipango yao hata ahadi za Fedha za Miradi hawaja ambulia, licha ya Uhuru Kenyatta kwenda China mwezi uliopita.

    -Wakati sisi Raisi wetu Mwana wa Tanzania JK Maraisi wote na Dunia XI JINPING-CHINA, OBAMA-MAREKANI, BUSH-MAREKANI, CLINTON-MAREKANI, TONNY BLAIR-UINGEREZA WAKIAMBATANA NA WAKE ZAO wote kwa pamoja, Wazito wengine wa nchi zingine tena 'Tajiri' za Dunia wamemfuata yeye JK kwake Dar Es Salaam na Kusaini naye Mikataba LUKUKI huku Fedha zikiwa tayari kwa Miradi kutekelezwa!

    -Kagame ana Akaunti ya Bahati ya WIZI WA MADINI MASHARIKI YA KONGO inayompa jeuri ya fedha ambayo tuseme imesha fungwa kutokana na Majeshi ya UN chini ya KOMANDI YA MAJESHI YA JWTZ YA TANZANIA hawana uwezo wa kuokota hata kokoto moja ya madini kwa sasa, hivyo uwezo wa Kifedha wa Kagame unaelekea ukingoni.

    -China wamesaini Mikataba ya Miradi mikubwa 14 na Fedha kuwekwa tayari kwa matekelezo ya MIRADI TANZANIA, wakati akina K3 fedha za kuendeshea Miradi yao kama hiyo LAPSSET Bandari na Lamu ndio sasa wanatapatapa na dunia huku wakiwa na Makesi kibao kibindoni na wote watatu hawakubaliki Kimataifa.

    -Obama na Marekani wamesaini Mikataba lukuki ya Miradi mikubwa sana ya miundo mbinu na Nishati US$ 7 Billion huku mingi ikielekezwa Tanzania ktk hii Afrika ya Mashariki.

    Hiki ndio kitu kinacho fanya wamtenge kwenye Vikao vya Miundombinu ni kuwa mewapiga MABAO VIKALI SANA!

    ReplyDelete
  8. Picha ya kwanza Kagame anajikakamua kicheko na tabasamu lakini inashindikana!

    Wakati Muungwana JK kicheko na roho safi ndio haiba zake!

    ReplyDelete
  9. ila mie namaindi kabiza japo kulipiza kisasi sio vyema ,unafikiri mpaka Rais wetu kweli kutukanwa vile kweli ujue na sie wapiga kura wake/watzanzani tumetukanwa pia kwani tuna mwamini kabisa,sasa jamani aangalie sie bado kikwete tunakuhitaji jembe letu lkn kukutana na adui wakati umefukuza M23 huko kongo hamwezi kuyamaliza kwa mdogo ,msuluhishi mwenyewe akiwa mseveni ambaye ndio wanafanya naye vikao bila wewe baba yetu rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania dokta,jakaya kikwete,,sera ya uhamiaji uendelee kama ilivyo.MSEVENI HAWEZI KUWA MSULUHISHI WAKATI YEYE NI RAFIKI WA ADUI YAKO..{THE FRIEND OF MY ENEMY HE IS ALSO MY ENEMY} TAKE CARE BABA YETU AISEE.

    ReplyDelete
  10. Kagame pamoja na kuchukia Ushauri wa JK lakini meseji sent!!!

    ReplyDelete
  11. Ni kawaida kwa Mgonjwa kuchukia Dawa ama Ushauri wa Dakitari.

    Dawa ni chungu na pia sindano zinauma.

    Kagame amechukia Dawa na Ushauri wa Dr. Jakaya Kiwkete!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...