Bibi Hilary Clinton akiteta jambo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kupiga picha ya pamoja na viongozi wengine  katika hafla ya kuweka mikakati ya kupambana na ujangili wa wanyama pori hususan Tembo katika nchi za Afrika iliyofanyika katika hoteli ya Sheraton jijini New York Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita. Mfuko wa Clinton Foundation utatoa msaada wa fedha kufanikisha mapambano dhidi ya ujangili katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Viongozi wengine wa Afrika waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda(kulia),Rais Joyce Banda wa Malawi(wa pili kushoto),Rais Alassane Outarra wa Ivory Coast(watatu kushoto),Rais Ali Omar Bongo wa Gabon(Wa nne kushoto) na Rais Blaise Compaore wa Burkina Fasso(wapili kulia). Watano kushoto aliyesimama ni Chelsea Clinton Binti wa Rais Clinton ambaye ni mwanaharakati dhidi ya Ujangili.Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...