Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wakati alipowasili katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuanza ziara ya kikazi 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya,iliyopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi,Mkoa wa Mwanza.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na bvaadhi ya watoto waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Shule ya Msingi Ntulya,katika kata ya Mondo,wilayani Misungwi
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba motto Paulo Muhangwa muda mfupi baada ya kuzindua shule ya Msingi Ntulya wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalmiana na baadhi ya wauguzi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo,
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezoi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Septemba 6, 2013, amefungua shule ya kisasa ya msingi ya Ntulya katika kata ya Mondo, Wilaya ya Misungwi, iliyotolewa kama zawadi kwa wanakijiji cha Ntulya na taasisi moja ya Marekani.

Aidha, Rais Kikwete amezindua huduma za x-ray kwenye Hospitali ya Wilaya ya Misungwi mjini Misungwi ikiwa ni hatua zake za mwanzo kwenye siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Rais Kikwete katika mkoa wa Mwanza ambako atakaa siku tano akikagua na kuzindua miradi na shughuli za maendeleo.

Shule ya Ntulya iliyoko kilomita 47 kutoka mjini Misungwi ina wanafunzi 466 na walimu 11 na ni zawadi ya Taasisi ya Africa School House ya Marekani kwa wanakijiji cha Ntulya ambako Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt. Aimee Bessire ambaye amehudhuria sherehe za uzinduzi wa shule hiyo na mume wake, Mark Bessire walipata kuishi wakifanya utafiti kuhusu utamaduni wa Kabila la Wasukuma.

Shule hiyo ya kisasa imejengwa kwa matofali ya kuchomwa na ilijengwa kati ya 2008 na 2010. Ina madarasa 11, nyumba 10 za walimu na kisima cha maji safi. Kwa jumla shule hiyo ina uwezo wa kuwa na wanafunzi 600 kwa wakati mmoja.

Akizungumza kwenye sherehe za leo, Dkt. Bessire ambaye amezungumza kwa ufasaha lugha za Kiingereza, Kiswahili na Kisukuma, amesema kuwa shule hiyo imejengwa kwa jumla ya sh bilioni 1.038, na kati ya hizo sh milioni 980 zilitolewa na Africa School House, Halmashauri ya Misungwi ilichangia sh milioni 28 na nguvu za wananchi zilichangia sh milioni 30.

Taasisi hiyo ya Marekani pia imewajengea wanakijiji hao wa Ntulya Kituo cha Afya kwenye eneo hilo la shule na Dkt. Bessire amesema kuwa Taasisi hiyo ina mipango ya kujenga shule ya mfano ya sekondari ya bweni ya wasichana.

Dkt. Bessire pia amesema kuwa yataanzishwa madarasa kwenye shule hiyo kwa ajili ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Raisi JK ni Jogoo wa Afrika ya Mashariki!!!

    Hawa Maraisi wa nchi za EAC akina K3 wamekuwa na harakati za kumtenga Raisi wetu kutokana na wao kufunikwa naye vibaya sana ktk kila Idara.

    Uwezo na kukubalika kwa Maraisi kunaakisi taratibu kama za Maksi za Wanafunzi wakiwa ktk Mitihani ya Masomo Darasani.

    Ufuatao ni Muhutasari wa Matokeo ya Maksi au Alama za Maraisi kama sehemu ya kipimo:


    WALIOPASI MASOMO NA MTIHANI:

    Nafasi RAISI MAKSI ALAMA
    1. JK 107% A+++
    2. Nkurunziza 49% C-


    ...........................


    WALIOFELI MASOMO NA MTIHANI:

    Nafasi RAISI MAKSI ALAMA
    3. UHURU K. 37% D+
    4. M-7 23% D--
    5. PAUL K. 7% F

    Hivyo Matokeo hayo hapo juu kwa Raisi alieshika Nafasi ya 5 (Paul K.) kwa kuchachwa na Mshindi wa Kwanza JK Maksi 100% zaidi ndio kilicho fanya awe amesononeka usoni alipokutana na Mshindi JK Jijini Kampala!

    Kagame amepata Maksi 7% (Namba ya Kiatu)

    Kufeli mchezo?

    ReplyDelete
  2. Raisi wa Afrika ni Mhe. JK !!!

    Hakuna siku nilikuwa na wasiwasi ni siku ya Kikao Uganda kwake kuonana na Raisi Kagame wa Rwanda, baada ya yeye Raisi JK akiwa anatokea kwenye Kikao cha Kimataifa cha UN na Umoja wa Ulaya huko Alpbach-Austria nilijua Kikaoni Kampala kutazuka Ngumi Ukumbini!

    Kubwa zaidi la woga wangu ni baada ya kusikia Raisi Uhuru Kenyatta na Raisi Pierre Nkurunzinza wa Burundi hawata kuwepo Kikaoni nilipta woga zaidi,,,lakini ahhh wapi Kikao kilimalizika na nikasikia Jioni yake ya kuwa Mambo yamewekwa sawa!!

    ReplyDelete
  3. ''MTWI WA ZUMBE UNA MAGWANDU GWANDU''

    Hayo ni maneno ambayo alitakiwa kuambia Chifu mmoja wa Kabila la Kizigua yakimaanisha ya kuwa ''KICHWA CHA MFALME KINA MIKUNJO MIKUNJO'' jambo ambalo kila mtua liogopa kumweleza Mfalme, ama walikuwa wana nong'ona chini chini, lakini akajitokeza mtu mmoja jasiri ndio akamweleza waziwazi Mfalme na wala hakuna alilofanyiwa ingawa Mfalme alikasirika lakini Ujumbe ukawa umefika.

    HAYO NDIYO YALIYOTOKEA BAADA YA MHE. RAISI JK KUMPA UKWELI RAISI KAGAME WA RWANDA KUKAA NA WAASI ILI WAONDOE TOFAUTI JAMBO AMBALO HATA WAKUBWA KAMA UN-UMOJA WA MATAIFA,NCHI ZA UMOJA ULAYA NA MAREKANI WALISITA KUMWELEZA !!!

    Hivyo Raisi JK ni Shujaa wa kweli.

    ReplyDelete
  4. Kila mgonjwa na Dakitari wake na kila mtu na Kinyozi wake.

    Dr. Jakaya Kikwete ni Dakitari wa watu wawili Maraisi korofi hapa Afrika Mama Joyce Banda na Paul Kagame.

    Mara zote mgonjwa anayepingana na ushauri wa Dakitari maradhi humtesa ama anaweza kufikwa na mauti.

    Dr.Kikwete Bingwa na Tiba amemshauri:

    1.Raisi Joyce Banda ya kuwa suluhisho la Kiuchumi nchini Malawi kwa njaa za mara kwa mara sio kulimiliki Ziwa lote la Nyasa bali atumie upande wa maji yake ktk ziwa kwa Tija na Mipango ataona mabadiliko.

    2.Raisi Paul Kagame ya kuwa aongee na Waasi kuondoa tofauti ili aiweke nchi yake ktk Amani na kuimarisha Uchumi zaidi,,,akachukia Ushauri kitu ambacho Kitaalamu kinakubalika kujenga mazingira mazuri zaidi Kiuchumi kama kutakuwa na Amani ua Kudumu ktk nchi na eneo letu lote.

    Tumeshuhudia Wagonjwa hao wawili Maraisi hapo juu waki kasirika kwa Ushauri wa Dakitari wao lakini kama watajirudi na waka tekeleza ushauri ni wazi watapona maradhi yao !!!


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...