LEO
UMETIMIZA MWAKA MMOJA KAMILI TOKA ULIPOTUACHA GHAFLA BAADA YA KUUGUA GHAFLA
SANA. HATUNA CHA KUSEMA TUNAAMINI UMEKWENDA KUTUANDALIA MAKAO YA MILELE ILI
SISI NASI TUKUTANE HUKO, MAANA HUKU DUNIANI TUKO MATEMBEZINI TU.
VICK
UMETUACHA KATIKA MAJONZI MAKUBWA NA MASWALI MENGI! KIFO CHAKO KIMETUSHTUA WENGI
MAANA KIMETOKEA MIEZI MIWILI TU BAADA YA HARUSI YAKO. LAKINI KWAKUWA TU
WAKRISTU TUNAAMINI MUNGU AMECHUMA UA ZURI KATIKA BUSTANI YAKE NA KAZI YAKE SIKU
ZOTE HAINA MAKOSA. TUMEKUBALI YOTE! TUPO KAMA ULIVYOTUACHA, TUNAENDELEA
KUKUENZI KWA HAYO INGAWAJE BADO MAJARIBU NI MENGI.
UNAKUMBUKWA
NA MIMI MAMA YAKO LYDIA, BABA JAPHET MBWANA, MUMEO MPENZI EMMANUEL KILATO, NDUGUZO
MERCY, GODFREY NA VIOLLA, MAMA MKUBWA, WAJOMBA, WAKWE ZAKO, WANA UKOO WOTE, MAJIRANI
WA LUMALA - MWANZA, GEITA NA DODOMA, WAFANYAKAZI BENKI KUU MWANZA, WANAJUMUIA
YA FIDEL – PAROKIA YA PASIANSI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.
MISA YA KUMALIZA MSIBA ITAKUWA NYUMBANI KWAO
LUMALA B TAREHE 7/9/2013 SIKU YA JUMAMOSI SAA NANE MCHANA, KARIBUNI SANA
RAHA YA
MILELE UMPE EEH! BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWNGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI
AMINA!
Liydia poleni sana Mungu aendelee kuwatieni nguvu na aendelee kuwafariji maana yeye ndie mfariji wa kweli
ReplyDelete