![]() |
Jackson M. Kalikumtima
Mwenyekiti Mtendaji
|
Shindano la Tanzania Top Model limeanzishwa ili kuziba ombwe lililoko la kuwatafuta, kuwatayarisha na kuwatafutia mikataba wanamitindo wa kitanzania ambao ndoto zao zimekuwa ni kufanikiwa na kuwa wanamitindo wa Kitaifa na Kimataifa. Ni shindano litakalo wajenga na kuwafanya wajiamini na waaminiwe kwa kazi mbalimbali. Hiki kitakuwa ni kichocheo kingine cha kuitangaza nchi yetu katika mavazi na sanaa nyingine kimataifa na kuwa chimbuko la nyota nyingine katika dunia ya Wanamitindo hapa nchini.
Mashindano ya kumtafuta Tanzania Top Model si mashindano ya kawaida kama tulivyo zoea mashindano ya kuwakutanisha Washiriki na kupima Mshiriki aliye bora tu kuliko wenzake, bali ni Mashindano ya kumtafuta Mwanamitindo bora tena wa Mfano hapa nchini. Haya ni mashindano yatakayo ruhusu Jamii/ Wananchi/ Wadau kushiriki kuchagua mshindi kwa kiwango Fulani. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...