Washiriki
wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiingia ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwa maandamano
ya kufunga maadhimisho Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani . Maadhimisho ya
Nenda kwa Usalama yamefungwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi
Gerson Lwenge baada ya kufunguliwa mwanzoni mwa wiki hii na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA
BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Kitengo cha Usalama na Mazingira kutoka Makao Makuu ya Wakala wa Barabarani Tanzania
(Tanroads), Zafarani Madayi akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge (wapili kushoto) jinsi Tanroads
inavyoweza kutengeneza barabara bora na zenye alama za usalama kwa lengo la
kuondoa ajali mbalimbali zinazoweza kutoa barabarani kabla ya kuyafunga
maonesho hayo yaliyokuwa yanafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini
Mwanza. Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti
wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima. Kauli mbiu ya Maadhimisho
ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha
na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, DCP Mohamed Mpinga, akikionesha
kitabu cha taaluma ya ufundishaji wa madereva kilichozinduliwa na mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, kabla ya kufunga
maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyokuwa yanafanyika jijini Mwanza. Kulia
(waliokaa) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la
Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu
ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Radio One, Deogratius Rweyunga (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira
Ame Silima, baada ya kupokea cheti cha kuthamini mchango wa Radio hiyo iliyopo
Dar es Salaam kwa kutangaza habari mbalimbali za usalama barabarani. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani yamefungwa rasmi na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi
Gerson Lwenge, jijini Mwanza leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA
BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...