Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe Lazaro Nyalandu aliongoza wadau wa utalii pamoja na wakazi wa Mwanza kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani inayosheherekewa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka.
Maadhimisho hayo kitaifa yalifanyika Jijini Mwanza na yalipambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo ufunguzi wa ofisi mpya ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa.
Ofisi hii imefunguliwa ili kukidhi mahitaji ya utangazaji wa utalii kwa Kanda ya Ziwa.
Akizungumza katika kilele cha Siku ya Utalii Duniani, Mhe Lazaro Nyalandu aliwaasa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii na kushangaa nchi yao. Akitumia maneno yaliyomo kwenye wimbo wa ‘Nakupenda Tanzania’ yasemayo “Tanzania Tanzania ninapokwenda Safarini, kutazama maajabu”
Alisema wimbo huu uliotungwa na wazee wa zamani ulionyesha hazina kubwa ya vivutio vilivyopo nchini na hivyo kuhamasisha utalii kwa wananchi wote.
UTALII NA MAJI: KULINDA HATMA YETU
Mhe Lazaro Nyalandu akiweka saini kitabu cha wageni wakati wa kufungua ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania, Kanda ya Ziwa.
Kikundi cha ngoma kutoka Bujora wakitumbuiza katika kilele hicho.
Asante
Mwanafunzi Zuberi Kihumbe akipokea zawadi baada ya kuibuka mshindi katika shindano la kuandika Insha inayohusu utalii. |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...