Ili kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa
Montreal, serikali imeandaa na kutekeleza programu ya Taifa ya kuondosha
matumizi ya kemikali haribifu kwa tabaka la ozoni.
Akiongea kwa Niaba ya ya
waziri wanchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira waziri mwenye dhamana ya
kushughulikia masuala ya Muungano Mh. Samia Hassan Suluhu alipozungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake leo, amesema mikakati ya kitaifa ndani ya
Programu hii ni pamoja na kujenga uwezo wa taasisi zinazosimamia utekelezaji wa
mkataba. , kutoa elimu kwa wadau na umma
wa watanzania kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari
zinazolikabili.
Mheshimiwa suluhu aliongeza kwa kusema kuwa
kubadilisha technolojia katika viwanda vinavyotumia kemikali haribifu na kutoa
mafunzo yanayolenga kuimarisha ujuzi katika sekta ya kuhudumia viyoyozi na majokofu na kuhamasisha na
kuhimiza matumizi ya kemikali na technolojia mbadala na rafiki kwa tabaka la
Ozoni ni njia ambazo serikali inatumia kunusuru kuharibika kwa tabaka la hewa
ya Ozoni
“Ni
muhimu tuzingatie kwamba juhudi za kila mmoja wetu zinatakiwa kupunguza na kuondosha
mathara katika Tabaka la Ozoni yanayo sababishwa na bidhaa tunazo nunua na
kutumia majumbani au sehemu za biashara alisisitiza.”
Mh Suluhu aliwaasa wananchi kushiriki katika
kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa kuzingatia
kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku, kuepuka kutupa ovyo
majokofu na viyoyozi chakavu ama vifaa vya kuzuia moto vyenye kemikali
zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni,
Alitoa wito kwa mafundi wa majokofu na
viyoyozi waakikishe kuwa wananasa kwa kutumia tena vipoozi (refrigerants) kutoka kwenye viyoyozi, na
majokofu wanayo hudumia badala ya kuviachia huru ili visisambae angani na
amewashauri mafundi hao watoe elimu kwa wateja wao juu ya njia raisi za
kutambua uvujaji wa vipoozi.
Maadhimisho hayo ya siku ya Ozoni duniani
ambayo huadhimishwa tarehe 19 ya mwezi wa September kila mwaka, mwaka huu
yatafanyika katika chuo cha VETA-Nyakato jijini Mwanza yakiambatana na
maonyesho ya bidhaa na technolojia mbadala na rafiki kwa Tabaka la Ozoni Pamoja
na mafunzo na njia bora za technologia sahahi ya kuuudumia viyoyozi, majokofu
na mitambo ya kupoozea viwandani.
Walengwa wakubwa wa maadhimisho haya ni
mafundi wa kuudumia majokofu viyoyozi mitambo ya kupoozea kutoka viwandani vya
kusindika minofu ya samaki vinywaji na taasisi za ufundi zenye fani ya kuudumia
majokofu na viyoyozi. Lengo kuu ni kuelimisha mafundi kuhusu technolojia mpya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...