Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Dar es Salaam katika hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Dar es Salaam katika hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wazanzibar wanaoishi Dar es Salaam, wajitokeza kumsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, katika hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungia mkono wananchi wakati akitoka katika ukumbi wa hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na Wazanzibari wanaoishi Dar es Salaam. (picha ya Salmin Said, OMKR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. miaka nenda rudi hawa wenzetu wanapenda kukutana start light. hivi Hivi Rais wetu akienda kutembelea zANZiBAR na akataka kuongea na watu wa mkoa wa pwani wanaoishi Zanzibar itakuwaje? si ataambiwa ni mbaguzi? tuwe makini. kama ni nje ya nchi sawa, lakini hata humu humu nchini? is too much

    ReplyDelete
  2. Je bado kuna Muungano? Taarifa hii inaeleza wazi kwa hao ni Zazibar wanaoishi Dar na siyo Watanzania. Kiongozi wao amesafiri kutoka Zanzibar kwenda Dar (Tanganyika) na kukutana na wananchi wake. Kama ambavyo viongozi wengine wanavyofanya wakienda nje ya Mipaka ya Tanzania. Huyu ni kiongozi mkubwa. Je taarifa hii imepewa jina hilo kwa bahati mbaya au inaujumbe kwa wale wanaodhani kuna Muungano.

    ReplyDelete
  3. Hivi ni Wazanzibari au ni Wapemba? Tuachane na siasa na tuzungumze uhalisia. Zanzibar ni Unguja na ndio maana hapo kale tuliwahi kuwa na Chama kilichoitwa Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP).

    ReplyDelete
  4. Kabla ya kulaumu inatupasa kujua kwanza kama alikuja Dar kama makamu wa rais, Katibu wa CUF au ziara binafsi?

    ReplyDelete
  5. Ni bora wajiandae maana kwa maoni yangu ukiangalia yanayofanyika huko bungeni, mikutano huko Zanzibar na Pemba; watu wakipiga kura hakuna muungao.

    Naona wanajiandaa kwa lolote.

    ReplyDelete
  6. ALIKUJA KUKUTANA NA CUF WENZAKE ..MIE MZANZIBARI LAKINI SIKUWA NA HABARI...HIVYO HABARI LABDA ILITOLEWA CHAMANI BUGURUNI..

    ReplyDelete
  7. Bado hamjajua tu muungano kwishnei? Kama mlikuwa bado, basi hizo ndizo dalili zake.

    ReplyDelete
  8. Yote na yasemwe, hawa jamaa zako huwa hawaishi kunung'unika. Hili limuungano na life cc tubaki Tanzania na wao Zanzibar watajiju kwani hakuna maana ya kuwa Tanganyika sababu waliozaliwa katika Tanzania ni wengi kuliko wa Tanganyika. Tanzania bila Zanzibar inawezekana na ni muhimu tene itapendeza

    ReplyDelete
  9. It does not sound good, Its strange

    ReplyDelete
  10. Kaenda kuwaarifu Wanankataba kuwa wajitayarishe kurudi Ntambwe maana muungano ukivunjika ndivyo mambo yatakavyokuwa.

    ReplyDelete
  11. Mhh langu jicho

    ReplyDelete
  12. tanzania bila ya zanzibar inawezekana au tanganyika bila ya zanzibar inawezekana???!

    acheni kupotosha historia bana. Sijui kwanini hampendi kutumia jina lenu la asili 'TANGANYIKA'!!!

    ReplyDelete
  13. Nimependa bango ktk picha ya kwanza lililoando Jumuia ya Wazanzibari waishio Tanganyika.

    Hii inadhiirisha wenzetu kutambua Muungano ni wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar ( Tan + Zan + ia = Tanzania).

    Nashangaa wadau wengine kutaharuki jina Tanganyika kutumika maana hata ktk articles za Muungano wa Tanzania zinaseama bayana ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

    Udumu Muungano wetu wa kweli wa damu maana tulianza kuwa na mashirikiano muda mrefu sana kabla ya mwaka 1964 Muungano wetu kuwekwa ktk wino na karatasi.

    Mdau
    Mtanzania

    ReplyDelete
  14. This is OUT OF ORDER ..simply put !!!

    ReplyDelete
  15. Kama ndugu zetu wa Visiwani hamridhiki na Muungano, mjiandae kufunga virago!

    Msitegemee muache Maduka yenu Bara na Mabasi ya Daladala Bara kazi ikiendelea huku mkija kuchukua MAHESABU, MJITAYARISHE KUONDOKA BARA NA KUJA BARA TENA MTAKUJA KWA PASIPOTI NA VIZA!

    ReplyDelete
  16. mutajiju,kwani kingwendu kamaliza.

    ReplyDelete
  17. Bila ya znz hakuna Tanzania kuna Tanganyika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...