MNAMO TAREHE 26.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO KATIKA MTEREMKO WA PIPE LINE INYALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA, GARI T.605 AXX /T.480 CAX AINA YA SCANIA LORI LIKITOKEA NCHINI ZAMBIA KUELEKEA DAR – ES SALAAM LIKIENDESHWA NA DEREVA WILSON MACHA, AKIWA NA UTINGO WAKE JUMA S/O SALEHE WOTE WAKAZI WA DSM [AMBAO KATIKA AJALI HIYO WOTE WAMEFARIKI DUNIA] LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL ARON, MIAKA 30, MKAZI WA SINZA, KISHA GARI HILO LILILIGONGA GARI T.876 BKV/T.465 BQU AINA YA IVECO LORI AMBALO LILIKUWA LIMEEGESHWA PEMBENI YA BARABARA LIKIWA LIMEHARIBIKA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL KASUSU, MIAKA 37, MJITA, MKAZI WA GONGO LA MBOTO DSM. 
AIDHA GARI HILO T.605 AXX /T.480 CAX LIKIWA LIMEPOTEZA MWELEKEO LILIGONGANA USO KWA USO NA GARI T.255 AKV/T.272 CDZ AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI AMBALO LILIKUWA LINAENDESHWA NA DEREVA SIXTUS S/O KAPINGA, MIAKA 35,MNGONI, MKAZI WA DSM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA MWILI WAKE KUTEKETEA KWA KUUNGUA MOTO.  
 KATIKA AJALI HIYO MAGARI MAWILI T.605 AXX /T.480 CAX NA T.255 AKV/T.272 CDZ YOTE YAMEUNGUA VICHWA NA KUTEKETEA NA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN LILIUNGUA KIDOGO SEHEMU YA KICHWA UPANDE WA KULIA. § CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.605 AXX /T.480 CAX. 
 MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI NA WANANCHI. § MIILI YA MAREHEMU WILSON MACHA NA JUMA SALEHE IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. JITIHADA ZA KUUTOA KATIKA GARI MWILI WA MAREHEMU SIXTUS S/O KAPINGA PAMOJA NA KUTOA MAGARI ENEO LA TUKIO ZINAENDELEA. 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 
 Signed By: [DIWANI ATHUMANI - ACP] 
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA. 
 PICHA NA MDAU WA MBEYA YETU
SEHEMU YA MABAKI YA MOJA YA MAGARI HAYO
MAGARI YAKIWAKA MOTO
ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO WAKIPAMBANA NA MOTO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Askari Polisi barabarani. Tuache kudai Milungula, tukague magari kwa usalama wa raia. Tuwe wazalendo.

    ReplyDelete
  2. Jamani Jamani, sasa huyu firefighter mwanmke ana casual shoes wakati wa kuzima moto, tutafika kweli. Poleni kwa ajali

    ReplyDelete
  3. mungu awaweke mahala pema marehemu wote inshaallah.

    ReplyDelete
  4. Poleni waliopata ajali,ila hapo kuna utata na huo moto,isije kuwa wajanja walishachukua mali zao na kuchoma magari moto.
    uaminifu hakuna siku hizi....

    ReplyDelete
  5. Noana kama ni shaba(copper) pembeni au???pia kuna container la Maersk Line sijui ndani kama vimesalimika vinavyosafirishwa!
    Jamaa washachukua chao wanasingizia moto.
    Mnakumbuka hata Bank zikiibiwa wanachoma moto.
    Bongo kila mtu anakula kivyake,yote maisha....

    ReplyDelete
  6. hv nyie wachangiaj wengne hua hamsomi maelezo mnacomment kwa kutumia pics tu ama inakuaje?!! yan mna kabisa kama hiyo ajali ni wote wamefariki, sasa wapange issue ya kuiba ili iweje? amuibie nani na wenyewe ni marehemu!?

    ReplyDelete
  7. Division 0 Ltd, zungumzieni uhai wa watu si mali na uzushi. Tufanyeje ajali za namna hii zisijirudie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...