Mike Mhagama "enzi" zake akiwa studio za Radio One Stereo/ Picha kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Mike Mhagama Michael Pesambili Mhagama ni mmoja wa watangazaji wa awali waliojikita katika harakati za kuutambua, kuuboresha na kuupa hadhi muziki ambao sasa unatambulika kama BONGO FLAVA. 
 Pia ndiye aliyeanzisha JINA hilo la Bongo Flava. Jumamosi ya Aug 31, 2013, alifanya mahojiano na JAMII PRODUCTION na kueleza mengi kuhusu Muziki huu wa Bongo Flava Ameeleza harakati zao kuuweka kwenye ramani ya muziki nchini, matatizo yanayoukabili, mafanikio na hata ambapo angependa kuuuona ukifika na kuwafikisha wahusika wake. 
 Unajua jina BONGO FLAVA lilipotoka na lilivyotokea? Alikabiliana vipi na UTATA WA MUASISI WA JINA BONGO FLAVA? Lakini je, ni yeye muasisi wa harakati za kuwa na muziki huu radioni? Anauonaje muziki huu? Unakua ama? Wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki huu nchini ni upi? Karibu uungane nasi NB: Tunaomba radhi kwa ubora wa sauti katika sehemu za mahojiano haya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mr Mhagama wewe umezaliwa Tanzania?
    unashangaa Dj Kuomba Rushwa?Kwa swala la Rushwa Tanzania ni Janga la Dunia.wenyewe tumesha kaa kimya.Tanzania tunahitaji kuingizwa kwenye Record ya Dunia kuna sehemu unaombwa Rushwa mpaka unaweza kuzimia.watu wa Redio ni wala Rushwa mapapa acha. Any way unapongezwa sana kwa Bongo Fleva.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...