Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 .  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea katika kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa Dkt. Edward Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho kilitoa zaidi ya vitabu  4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John McLaughlin. Picha na John Lukuwi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. this is how mwanamke kiongozi dresses, good on you First Lady. Truly proud of you

    ReplyDelete
  2. Huyu mama mara nyingi anapendeza sana.

    ReplyDelete
  3. Eh mwalimu Salma weee, hongera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...