-Na Freddy Macha
LOGO -fashion Sept 7- by Sara Abood 
  Mchoro wa shughuli uliobuniwa na Sara Abood. 

Wabunifu mavazi wanne toka Tanzania walioshiriki maonesho ya mavazi Ubalozi wetu London Jumamosi Septemba Saba wamechaguliwa kuingia dimba la kimataifa London Fashion Week, Februari mwakani. Wasanii hao waliopewa nafasi ya kujitangaza kupitia jitihada za Jumuiya ya Wanawake Uingereza (TAWA) ukishirikiana na Ubalozi ni mseto wa wafanyabiashara wakongwe na vijana wanaoanza fani hii ya urembo. Mama Joyce Kallaghe-pic by Felipe Camacho 
  Mama Joyce Kallaghe, ni mtangazaji mzuri wa mavazi ya Kitanzania ughaibuni. Picha na Felipe Camacho. Akifungua shughuli hii, mkewe Balozi, Mama Joyce Kallaghe alikumbusha hii ni nafasi nzuri kwetu. “ London Fashion Week” ni tafrija maarufu inayofanyika sambamba Paris, New York, Milan mwezi Februari na Septemba kila mwaka toka 1984. Mbali na msaada wa TAWA na Ubalozi, mwekezaji mkuu wa shughuli hii ni British Council- shirika linaloendeleza vipaji nchi zaidi ya 100 duniani kwa miaka 75 sasa. Mada ya maonesho iliitwa “Fahari Passion 2013” na mchoro wake uliobuniwa na Bi. Sara Abood unaonyesha uso wa mwanamke na rangi za bendera ya taifa.
Khanga dress tight 
Khanga inavyojigamba na kupendeza. Picha na Abubakar Faraji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...