Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili inayojumuisha Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Mameneja wa Majengo wanahudhuria warsha ya siku mbili inayohusu usimamizi na uboreshaji wa huduma za Hospitali.
Katika warsha hii, jumla ya mada tano zitatolewa ikiwemo jinsi ya kupambana na vitendo vya rushwa katika mahali pa kazi hususani katika sekta ya afya, jinsi ya kusimamia kanuni na taratibu mbalimbali kufanya kazi na kufanya maamuzi, jinsi ya kujenga umoja na kusimamia dira pamoja na tunu za Hospitali.
Warsha hii imeandaliwa kwa nia ya kuwakumbusha Timu ya Menejimenti majukumu yao kama viongozi wa Hospitali katika kutekeleza majukumu waliyopewa ikiwemo kuhakikisha utendaji kazi unasimamiwa vizuri kwa mujibu wa taratibu na kanuni za kazi, viongozi kusimamia wafanyakazi walioko chini yao ili kuongeza tija na huduma bora kwa wananchi.
Warsha hii inaendeshwa na taasisi ya mafunzo kwa viongozi (Institute of Directors in Tanzania IDT) na inafanyika Jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Landmark iliyoko Mbezi Beach.
Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kutoka kulia Dkt. Kassim Hussein mwezeshaji wa warsha akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa IDT Bw. Said Kambi, anayefuata ni Dkt. Marina Njelekela Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akifuatiwa na Bw. Makwaia Makani Mkurugenzi wa Utumishi na Bi. Agnes Mtawa Mkurugenzi wa Uuguzi wote kutoka MNH.
Aliyesimama ni Mwezeshaji kutoka Takukuru Dkt. Kihiyo akitoa mada kuhusu namna ya kupambana na rushwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
TUNATEHEMEA UTENDAJI BORA KATIKA HOSPITALI BAADA YA MAFUNZO HAYA
ReplyDeleteHapo kifuatacho sasa ni utendaji ndicho kinacho ngojewa na wananchi
ReplyDelete