DHL_5976
Wakati upepo mzuri wa kipindi cha joto kutoka bahari ya Hindi ukipuliza, uzinduzi wa mgahawa mjini Zanzibar, Six Degrees South, ulikuwa hauna mfano! Huku kukiwa na fataki za ndani, chupa za Moet zikifunguliwa kwa madaha usiku kucha mpaka mida ya usubuhi, uzinduzi wa Six Degrees South uliwaacha wengi mjini Zanzibar wamepigwa na butwa wakiwa hawana la kusema.
PBF_6038
DHL_5927
Six Degrees South ipo eneo la mji mkongwe na inawapa wageni utulivu wa hali ya juu ili kuwawezesha kupumzika na kujichanganya. Ukichanganya mazingira ya utulivu na na huduma ya bure ya mtandao wa internet, sehemu hii inamfaa mtu yoyote kupata kinywaji anachopendelea na vitafunwa. Mgahawa una vibaraza kwenye ghorofa tatu vyenye eneo kubwa kwa ajili ya wageni kutazama jua likizima kwenye mandhari ya Bahari ya Hindi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mji mkongwe ni mkubwa, sema hasa ni sehemu gani ya mji mkongwe ulipo mgahawa huu!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Hizo picha za mwisho inaonekana ni pale zanzibar house,karibu na wizara ya utumishi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...