Ningependa kuwauliza wale watanzania walio Marekani kama tunaweza ku-share ni kadi gani za simu zenye dakika nyingi kupiga Bongo cell phones. Wengi wetu kupiga simu nyumbani ni muhimu, sio kila siku ila mara kwa mara. Na gharama za kadi kiasi fulani ni kubwa, mimi kadi ambazo natumia online nyingi ni 17c per minute (.17/min).. which means unapata karibia dakika 58 kwa $10.. Naelewa kuna apps kama viber ambazo zinasaidia kiasi fulani, ila ni vigumu kumwambia bibi akiwa Masasi kwamba weka viber kwenye simu.
Kwa hiyo kama mtu anajua website gani wana kadi zenye deal zenye rates nzuri kupiga Tanzania please naomba tuambizane. Kama itakuwa ya mtanzania itakuwa bora zaidi, kuinuana muhimu. Au kama kuna means za kupiga simu besides kadi mtu unajua please let us share.
Napatikana jmakwanga@yahoo.com


Natumiaga hii:
ReplyDeletewww.ezcalls.com
Rates zake ni different kutokana na mtandao utakaopiga kwa mfano kwa Tigo unaweza kuongea dakika 111 kwa dola 10.
Natumaini hii itakusaidia.
Kutoka kwa,
dailylifeandliving.blogspot.com
mdau makwanga ukweli wa mambo ulimwengu mzima VOCHA-TIGO ndo rahisi kinachotakiwa wajipange next-level kujinoa na mtandao wa kadi za kitaifa ndani na kimataifa kwa soko la nje haswa kwenu usa wadau wa bongo wapo wengi.
ReplyDeletemikidadi-denmark
Mimi natumia vip communications
ReplyDeleteTumia Umojaphone
ReplyDeletejaribu www.rebtel.com also ina rate nzuri na ni rahisi kuongezea hela.
ReplyDeleteboss revolution $5-voda 55min,tigo 34min,airtel 20min
ReplyDeleteBass revolution" igoogle hiyo iko poa
ReplyDeletekadi? we no longer use that where I am. That was about 10 years ago.
ReplyDeleteWhat is it actually?
UNAPIGA SIMU BONGO UNATAFUTA NINI?KURUDIA VUMBI?PIGA UK.
ReplyDeleteTabu Tanzania inachaji pesa nyingi kampuni hizi zilizo bei poa, inashangaza rates za kupiga TZ hata Europe wenzetu wakenya na waganda kwa dakika moja kwetu kuongea either mobile au landline. Wao ni mara tatu au nne madakika kwa bei hiyo hiyo.
ReplyDeleteTanzania inabidi ipunguze kuwachaji pesa nyingi hizi kampuni ili watupunguzie bei za kupiga per minute.
Mdau,hotvoip unaweza kupiga kwenda mitandao yote ya simu za mkononi Tanzania kwa gharama ya dola za kimarekani 0.068 kwa dakika,unachotakiwa ni kudownload hiyo software kisha kujisajili na kisha unanunua credits na baada ya hapo unaweza kupiga simu.
ReplyDeletekama unatumia Boost mobile, basi lipa zaidi kidogo ya bill yako na utapiga bila kutafuta CARD ZA SIMU ni kuinua tu na kubonyeza namba na inadumu muda mrefu karibu siku 15 hata kama unapiga kilasiku dakika mbili au jiunge na Westen union, kwa kutuma hela tu huko Tanzania, pia wanakuwekea AIRTIME kwenye card yao ambayo utatumia kama vocha na inadumu muda mrefu na conection yake ni beautiful.
ReplyDeleteSasa, bongo si wana mtandao? na simu karibu zote zina mtandao Bongo. Kwa nini utumie makadi tena wakati kama wote wawili mna download SKYPE, WHATSAPP, Yahoo messenger, LINE, VIBER, WECHAT, mnaweza kuongea BURE na kama simu zao ni smartphone, hata unaweza kuongea huku unawaona. Hizi mikadi yamepitwa na wakati.
ReplyDeleteumeshaambiwa bibi hawezi kuweka hozo viber stuff!
ReplyDeletekwa haraka nmepitia options zilizotolewa na inaonekana amantel.com wapo juu!
ReplyDeleteNunua MAgic JAck na huku mnunulie mtu MAgic JAck utaongea weee mbaka baaasi
ReplyDeleteAcha ubahili wanunulie ndugu/jamaa zako smart phones. Initial cost itakuwa kubwa lakini wakisha kuwa na smart phones, internet kwa simu Tanzania ni bei sawa na bure. Kwa hiyo wakishakuwa na smartphones, utasahau kununua kadi, na maisha yataenda vizuri. Mimi nilifanya hivyo, ndugu/marafiki zangu ambao natakiwa kuongea nao mara kwa mara niliwapatia zawadi za smart phones. Kwa kufanya hivyo niliokoa pesa nyingi ambayo ningetumia kununua kadi. Maana najua hauwezi kuwa na ndugu wa kuwasiliana nao zaidi ya kumi. Utakuwa na ndugu wengi lakini si lazima uwasiliane na wote.
ReplyDeleteKwa kutumia kadi unaweza kutumia USD 10 kwa siku. Kwa mwezi ni USD 300. Kwa hapa ninakoishi (Sweden) kiasi hicho cha pesa kinatosha kununua simu 3 ambazo unaweza kudownload viber, skype, n.k.
Ákili ni nywele..........
ReplyDeleteAkili ni nywele...., kila mtu ana kipara.
Makwanga acha kuichungulia Sarafu ya DOLA kama hivyo!
ReplyDeleteUnautia aibu Ugenini, ni kuwa gharama za maisha ni dunia nzima huwezi kuishi CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU KAMA UPO AFRIKA kumbuka upo Marekani kwa Obama!!!
Ndugu Makwanga hivi wewe utakuwa unatokea mkoa wa Kilimanjaro?
ReplyDeleteUna onekana Mchumi sana!
Makwanga upo Marekani kwa muda mrefu sana!
ReplyDeleteKama unataka msaada wa mawazo kwa nini usipige Simu namba 911 upate majibu?