Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukiwa tayari kwa kuagwa Hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam,na kuanza kwa safari ya mazishi yatakayofanyika kijiji cha Nzasa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Mtoto wa Marehemu Baraka Simon(12)akimuaga mama yake mzazi kabla ya safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi kuanza aliemshikilia ni mama yake mkubwa Lucy Ngorido.
Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Yusta Mkali likiwa kwenye gari tayari kwa kuanza safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi yatakayofanyika hapo kesho.
| Wakinamama wakilia kwa uchungu |
Mtuhumiwa Musa Senkando ambaye bado anatafutwa na Polisi kwa mahojiano akiwa mtuhumiwa wa mauaji hayo. Wananchi tunaomba msaada wenu kwani huyu mtu ni hatari sana katika jamii yetu.


huyo jamaa aliyemua huyu dada nihatari kwa taifa hili.tukimuachia aendelee kukaa na jamii nisawa kumfuga mtoto wa simba,ataua tena atakua wewe unaemuhifadhiukumbuke umemwaga damu hata ufanye nini utamwaga damu ya mwingine itakua mazoe yako kila kukicha unataka kuona damu
ReplyDeletekaka michuzi nimependa jinsi unavyoreport habari ya kifo, hasa katika kuweka picha (unamuhifadhi marehemu), bloggers wajifunze kutoka kwako, watu wanaweka picha ya maiti hadharani, yaani hakuna kuhifadhi wala heshima kwa marehemu, wao bora wauze habari. Mkuu ubarikiwe sana, na uendelee kuwalinda wale wasioweza kujilinda (marehemu)
ReplyDeletewewe anoy. wa pili unaogopa maiti? nini cha ajabu? Bro Michu wewe weka tu ndio safari ya wote.
ReplyDeleteUnknown wa pili yuko right..
ReplyDeleteSi vizuri kuanika sura ya marehemu hadharani kila mtu kupita na kumchora,kwani alivyokuwa hai mbona ulikuwa humtizami namna hile...hata yeye asingekubali kufanywa kituko kwa watu wapiti eti wanaaga,hata aliyekuwa adui wake pia anapita kwa kumkebei...
Ndio maana katika Dini yetu ya Kiislam maiti haifunuliwi hadharani,kwani mtu akishakufa hana jinzi ya kujitetea,sasa kwa nini umzalilishe???Mdau Mnyalu katafakari kwanza
Hanny London
Kwa yeyote aliyesomea na kufuzu uandishi wa habari kamwe hatoweza kuonesha matukio kama ya vifo visivyo vya kawaida hadharani na itakapobidi kufanya hivyo basi ni lazima aiombe radhi hadhira yake kabla; hivyo ndio media ethics zinavyotaka, sasa wewe unayesema lazima maiti zioneshwe mimi sikushangai kwa vile huna unalojua kuhusiana na hii fani ya kupashana habari!!!
ReplyDeletePia sio busara hata kidogo kwa watoto chini ya miaka 18 kuoneshwa maiti hata kama ni za wazazi wao kwa vile tukio hili lina athari ya kudumu kisaikolojia.