Naibu waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum mwishoni mwa juma alifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara za Kaskazini Pemba zenye urefu wa Kilomita 35. Ujenzi wa barabara hizi unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia programu ya Milennium Challenge Account – Tanzania (MCA-T) kwa thamani ya shilingi bilioni 38.2.
Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi ulisainiwa tarehe 18 August, 2011 na unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya H. Young & Co(E.A) Ltd.
Ujenzi huu unajumuisha barabara za Kipangani - Kangagani (km 2.7), Chwale- Likoni (km 1.9), Mzambarauni Takao- Finya (km 7.9), Mzambarauni Karim - Mapofu (km 8.7), Bahanasa - Daya (km 6.7) na Makongeni – Daya - Mtambwe (km 7.1).
Utekelezaji wa miradi hii uko katika hatua za kukamilika ambapo awali mradi huu ulitakiwa ukamilike tarehe 21 Machi, 2013 lakini kutokana na “contractor” ameomba aongezewe muda wa kukamilisha hadi tarehe 26 Desemba, 2013.
Aidha, katika ziara hii Mhe. Naibu Waziri aliambatana na Mhe. Rajabu M. Mohamed (Mbunge wa Ole), Mhe. Haroub M. Shamin (Mbunge wa Chonga), Mhe. Rukia K. Ahmed (Mbunge Viti Maalum), Watendaji kutoka MCA-T, Wizara ya Fedha na Miundombinu – SMZ.
Wizara ya Fedha ya Serikali ya Muungano wa Tanzania ndiyo yenye jukumu la kuratibu utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa kupitia programu ya Milennium Challenge Account – Tanzania (MCA-T).
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Saada M. Salum akimsikiliza mkandarasi wa ujenzi wa barabara za Kaskazini Pemba na mwakilishi wa Kampuni ya LASA moja ya kampuni zinazotekeleza mradi huu ndugu R.D Sharma kuhusu ujenzi unavyoendelea.
Ndugu R.D Sharma wa wa Kampuni ya LASA, akitoa ufafanuzi wa baadhi ya
masuala mbele ya Mhe. Naibu Waziri
: Injinia Salum Sasillo
(aliyesimama) kutoka MCA-T akitoa ufafanuzi. Injinia Sasillo ndiye mratibu wa
utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara chini ya programu ya MCA-T
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...