TIMU ya soka ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mwishoni mwa wiki iliifunga iliyokuwa timu ya zamani ya shirika hilo, Shirika la Akiba ya Wafanyakazi (NPF), mabao 2-1 kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulianza kwa kasi na dakika ya tano ya mchezo, NSSF walikosa bao kupitia kwa Ally Sham baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mahadhi Mohamoud.
NPF walijibu shambulizi hilo dakika ya 15 baada ya Juju Mtukuru kuwatoka mabeki wa NSSF na kuachia shuti kali lilodakwa na kipa Abubaka Soud.
Salehe Biboze aliipatia NSSF bao la kwanza dakika ya 55, kabla ya NPF kusawazisha dakika ya 67 kwa bao la Prosper Lyoba huku Khalid Jambia akipachika bao la yshindi dakika ya 79.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu alisema madhumuni ya mchezo huo, ni kuweka mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha afya zao.
Beki wa NSSF, Kitwana Kidatu (kulia) akiwania mpira huku akizomgwa na mshambuliaji wa NPF katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa TTC Chang'ombe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...