Askari wa jeshi la polisi Afande Mwijage akitoa somo la Uraia kwa watoto waliyokuja kuiangalia helikopta kijiji cha  Benako wakati wa Doria ya kusaka wahamiaji haramu na mifugo yao  katika pori la Kimisi Wilayani Ngara leo asubuhi, ikiwa ni mwendelezo wa awamu ya pili ya Opereshani Kimbunga ambayo imeshaanza .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Serikali DUME!,
    Usalama na Polisi zinatishaaa!,

    Ni jukumu la muhimu ambalo Serikali inalifanya kuhusu Wahamiaji Haramu kwa ajili ya usalama na Ustawi wetu nchini.

    Ndugu zangu Waanzania BORA LAWAMA KULIKO FEHDEHA.

    Wahamiaji Haramu mara zote ni watu hatari sana kwa ustawi na usalama wa nchi na jamii kwa ujumla Wahenga walisema 'Msafiri Kafiri' ni kuwa Wahamiaji haramu ni kama wasafiri wapiti njia hawana uzalendo wowote kwa nchi na hivyo wanaweza kuihduru nchi!

    ANGALIENI MAAFA MAKUBWA YALIYOTOKEA NAIROBI-KENYA, KWA MAGAIDI WA AL-SHABAB NI MATOKEO YA KUWAKINGIA KIFUA WAHAMIAJI HAO HAO HARAMU!!!

    ReplyDelete
  2. Tunakushukuru sana Rais wetu Kikwete,wanajeshi na serikali yetu kwa ujumla, angalau mmetusikia kilio chetu watu wa Ngara. Hawa watu wametutesa sana sana mpaka tukawa kama watoto yatima wasiokuwa na mtetezi wala mlinzi.Wametuua sana misituni na kuteka magari ya watu binafsi na abiria.Tunaomba hili zoezi liwe endelevu maana wanatukejeli eti sisi watanzania hatuwawezi kazi eti hili zoezi ni nguvu ya soda litaisha na watarudi tu.Ila tunaomba muwaangalie na watu wa uhamiaji pamoja na viongozi wa vijiji na polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine kuwalea sana hawa wahamiaji.MUNGU ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  3. kazi nzuri serikali watanzania wote tuko nyuma yenu,timua wote hao manyang'au

    ReplyDelete
  4. wahamiaji sio wauza kahawa tu,wachunguzeni hadi maofisini. Mh Rais Kikwete kwakweli hongera sana kwa kufanya uamuzi huo maana hao ndio watakao haribu sifa ya nchi yetu yenye amani.

    ReplyDelete
  5. Sawa kabisa lakini mbona hawa wachina hawakamatwi na kurudishwa kwao.Wameja tele kila mahali wanauza mpaka chips na kuetengeneza magari tunaomba serikasli iwaangalie sivyo itakuja kuwa balaa.

    ReplyDelete
  6. Wachina hawawezi kuguswa. wameishainunua TZ. Inachekesha sana. Hili zoezi mpaka rais aingilie kati? ina maana waliowekwa kulinda sharia za nchi hawakufanya kazi yao vema.

    Uzembe utabaki pale pale. Na hawa wahamiaji wameshasoma udhaifu wa Tz ndio maana wanaambiana kuwa waende watarudi kwa kuwa Tz huwa na nguvu ya soda sio kama Kagame

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...