Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuhusu mkutano wa hadhara wa kuhamasisha wananchi kuhusu mchakato wa katiba mpya katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrajim Lipumba akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makubaliano yao na Jeshi la Polisi kuhusu Mkutano wao utakaofanyika katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
IGP, Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari.
Karibuni uwanja ni wenu, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema akiwakaribisha viongozi wakuu wa vyama vitatu vya upinzani mbele ya waandishi ya habari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ofisini kwake.
IGP, Said Mwema akiwashukuru viongozi wa vyama vya upinzani waliofika kwa mazungumzo ofisini kwake. Kushoto ni Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekityi wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akipongezana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Picha Zote na Francis Dandee
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...