Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha Star TV Abdala Tilata akishauriana jambo na Meneja wa Vodacom wilaya ya Missungwi Gift Tesha(katikati) na MenejaUhusiano wa Nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim muda mfupi kabla ya Vodacom kukabidhi vifaa vya michezo kwa shule ya MsingiLukungu iliyopo Wilayani Missungiwi Mkoani Mwanza.
MenejaUhusiano wa Njewa Vodacom Salum Mwalim akiongea kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa shule ya Msingi Lukugu iliyopo Wilaya ya Missungwi mkani Mwanza. Kushoto kwake ni Meneja wa Vodacom Missungwi Gift Tesha na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Kishiwa Maleba (wapilikushoto).
Meneja wa Vodacom Wilaya ya Missungwi Gift Tesha akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lukungu jezi zilizotolewa na Vodacom.Kampuni hiyo imeipatia shule hiyo jezi za mpira wa pete na soka pamoja na mipira ili kuendeleza michezo shuleni hapo ya kukuza michezo nchini. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Meneja Uhusiano wa Njewa Vodacom Salum Mwalim akimkabidhi Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Msingi Lukungu iliyopo Wilaya ya Missungwi Vicent Ndulu moja ya mipira iliyotolewa na Vodacom pamoja na jezi kuendeleza michezo shuleni hapo. Katikati ni Menejawa Vodacom Missungwi Gift Tesha.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lukungu iliyopo Wilaya ya Missungi Mkoani Mwanza wakifurahia kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni yaVodacom walivyokabidhiwa ilikushiriki vema katika shughuli za michezo wawepo shuleni. Vifaa vilivyotolewa ni jezi seti mbili za mpira wa soka, seti moja ya mpira wa pete, mipira na fulana za mazoezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...