Familia ya Marehemu Chief Shaaban Mtengeti II, inasikitika kutangaza kifo cha shangazi yao mpendwa Mama Rose Heinrich Sangiwa Mataji, mama yake Robin, Henry na Robert, kilichotokea Jumamosi tarehe 28 September alasiri huko Rochester, New York, Marekani.
Habari ziwafikie ukoo wote wa Mzee Heinrich Sangiwa, Bakari Sangiwa, Athumani Sangiwa, Mtengeti Sangiwa,  Kihama Sangiwa, Koshuma Sangiwa, Profesa Twalib Ngoma na ukoo  wote wa kina Ngoma,  na wa kwa Mdimu wote, na ukoo wa Rtd. Col. Julius Mataji wa Dodoma.
Mipango ya mazishi inafanywa huko Rochester, New York. 
Kwa Dar es Salaam ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu watakutana nyumbani kwa Bi. Hajjat Mwatumu Jasmine Malale,
51 Mlingotini Close,
Regent Estate,
Dar es Salaam
Jumatatu Septemba 30, jioni baada ya saa za kazi.
Kwa mawasiliano simu

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tunawapa pole wafiwa wote hasa watoto wake, mama mzazi, wadogo zake na familia yake waliopo Kisangara, Mwanga, kaka zake wa Mwanga, Moshi, Morogoro, Arusha na familia nzima ya Mzee Heinrich Sangiwa. Mungu amlaze pema mpendwa shangazi Rose.

    ReplyDelete
  2. Oooh poleni sana familia ya Sangiwa! Mungu amlaze pema mama yetu huyu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...