Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Fatima Chohan ( kushoto)  akisaini Hati ya Makubaliano ya mashirikiano katika masuala yanayohusu shughuli za Uhamiaji na Wakimbizi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi  leo Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini jana, watatu kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mh. Amme Silima aliyekuwa mwenyeji wa ugeni huu.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mh. Amme Silima  wa kwanza kushoto na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Fatima Chohan wa kwanza kutoka kushoto  wakibadilishana  Hati ya Makubaliano ya Mashirikiano katika masuala yanayohusu shughuli za Uhamiaji na Wakimbizi katika hafla fupi iliyofanyika leo katika ofisi za wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi, hafla iliyoshuhudiwa na Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbarak Abdulwakil pamoja na watendaji wa wizara hizo Tanzania na Afrika Kusini
Wajumbe wa Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Uhamiaji na Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania na  Wizara ya Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao cha wataalamu wa wizara hizo mbili ambapo walijadili maeneo mbalimbali watakayoshirikiana kwa pamoja.watatu kutoka kulia ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mh. Amme Silima na watatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Fatima Chohan wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbarak Abdulwakil.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Picha ya kwanza hapo juu imenikumbusha mbali kweli, yaani enzi za shule,ni kama vile kuna mtu anapiga chabo......

    ReplyDelete
  2. Mbona kama vile tunatazamia????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...