Wachezaji wa timu ya Netiboli ya Utumishi na TASWA QEENS wakigombea mpira wakati wa mechi ya kirafiki iliyofanyika jana katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Utumishi iliibuka mshindi kwa mabao 43-19.
Mchezaji wa timu ya Netobili ya Utumishi Anna Msolwa (kushoto) akitoa pasi wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Utumishi na TASWA QEENS katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.Utumishi iliibuka mshindi kwa mabao 43-19.
Mojawapo ya magoli ambapo Utumishi iliibuka mshindi kwa mabao 43-19 dhidi ya TASWA QEENS.
Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu (katikati) akiwapongeza wachezaji wa TASWA QEENS baada ya mechi ya kirafiki iliyofanyika jana viwanja vya Leaders Club kati yake na Utumishi.
----------------------------
Timu
ya Netiboli ya Utumishi imeendelea kujiweka sawa katika maandalizi ya
mashindano ya SHIMIWI baada ya kuichapa TASWA Queens mabao 43 kwa 19 katika
mechi ya kirafiki iliyokuwa na ushindani mkali iliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam jana jioni.
Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani wa aina yake,
ilianza kwa kasi huku wachezaji wa pande zote mbili wakioneshana umahiri wao .
Iliwachukua
takribani dakika 8 timu ya Utumishi kuumiliki mchezo katika kipindi cha kwanza na
kubwagiza TASWA Queens mabao 22 kwa 10.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi ya kushambuliana kwa zamu huku kila timu ikitaka
kujivunia idadi kubwa ya magoli mapema, ni Utumishi ndio walionufaika na mashambulizi
hayo baada ya kufika kwenye goli la wapinzani mara 25 na kufanikiwa kupata mabao
21 bila ajizi.
Kwa
upande wa TASWA Queens walifanya mashambulizi ya kutosha lakini ukosefu wa
umakini wa GA na GS wao uliwagharimu, hivyo hadi mchezo
unamalizika Utumishi waliibuka na ushindi mnono wa magoli 43-19.
Wafungaji
wa timu ya Utumishi walikuwa ni Fatma Ahmed aliyefunga mabao 25 na Anna Msulwa
aliyefunga mabao 18.
Kwa
upande wa timu ya TASWA wafungaji walikuwa ni Zainabu Ramadhani ambaye alifunga
mabao 15 na Elizabeth Mbasa ambaye alifunga mabao 4.
Akizungumza
baada ya kumalizika kwa mchezo huo Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma B.HAB Mkwizu alisema timu ya Utumishi inatakiwa iongeze
muda wa kufanya mazoezi zaidi ili iweze kufanya vizuri katika mashindano ya SHIMIWI
yajayo yanayotarajiwa kufanyika Septemba
hii mjini Dodoma.
“Muongeze
muda wa mazoezi ili mjiongezee stamina na pumzi ya kutosha kwa ajili ya mechi
zijazo”alisema Bw.Mkwizu.
Aidha,
Bw.Mkwizu alimtaka kocha wa timu hiyo Bw.Mathew Kambona kufanya marekebisho ya
makosa ya kiufundi yaliyojitokeza
uwanjani wakati wa mechi hiyo ili kuijenga timu kiufundi.
Naye
kocha mchezaji wa TASWA Queens Bi. Zainabu Ramadhani mara baada ya kumalizika
kwa mchezo huo aliipongeza timu ya Utumishi kwa kuwa na wachezaji wazuri na kuitaka timu hiyo kujiimarisha zaidi
katika upande wa ulinzi.
Timu
ya Utumishi iko kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kushiriki mashindano
ya SHIMIWI yanayohusisha watumishi wa Idara za Serikali na Wizara
yatakayofanyika viwanja vya UDOM
mjini Dodoma hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...