1

Wachezaji wa Waizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa wamembeba Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Ole Sante Gabriel kusherehekea ushindi walioupata timu za kuvuta kamba za wizara hiyo2Mshambuliaji wa timu ya mpira wa pete Hadija Jaha akijiandaa kutoa pasi kwa mwenzake wakati walipokutana na timu ya Wizara ya Maji. Wizara ya Habari ilishinda kwa alama 19 kwa 15.3Kiungo wa timu ya mpira wa pete ya Wazara ya Habari Flora Mwakasala akijiandaa kutoa pasi kwa mshambuliaji wa timu hiyo Grace Kingalame, wakati timu hizo zilipokutana katika mashinfdano ya SHIMIWI.4Kiungo wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari Mbozi Katala akimtoka beki wa timu ya Wizara ya Maji wakati timu hizo zilipokutana katika mshindano ya SHIMIWI.Habari ilishindwa kwa 1-05Wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya Wanawake ya Wizara ya Habari wakiivuta timu ya Afrika Mashariki (haipo pichani) katika mchezo wa mashindano ya SHIMIWI Septemba 22.
Hussein Makame, MAELEZO-Dodoma
TIMU za mpira wa miguu, pete na kuvuta kamba za  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo zimeanza vyema mashindano ya Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) baada ya kushinda michezo yao ya kwanza kwenye  mashindano hayo iliyochezwa Septemba 22 mwaka huu.
Timu ya mchezo wa kuvuta kamba ndiyo iliyoanza kufungua mlango wa ushindi kwa Wizara hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mivuti 2-0 kwa kuishinda Wizara ya Afrika Mashariki huku ikishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Ole Sante Gabriel.
Baadaye timu ya mpira wa miguu ilifungua pazia la michezo yake kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa bao la ushindi lililofungwa na James Mapepele aliyemchambua kipa wa timu ya Ardhi na kuiandikia timu yake goli pekee la mchezo huo.
Mchezo huo ulikuwa wa kuvutia kufuatia timu ya Wizara ya Ardhi kuonesha upinzani mkubwa lakini uimara wa kikosi cha Wizara ya Habari uliiwezesha kudhibiti upinzani huo na hatimaye kujihakikishia ushindi huo ambao pia ulichagizwa na Naibu Katibu Mkuu Gabriel aliyeitembelea timu hiyo majira ya asubuhi.
Kwa upande wa timu ya  mpira wa pete ya Wizara hiyo, iliibuka na ushindi katika mchezo wake wa ufunguzi baada ya kuitandika timu ya Wizara ya Maji kwa alama 19 kwa 15 baada ya safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Grace Kingalame kufanya kazi nzuri.
Naibu Katibu Mkuu Gabriel ambaye alihudhuria siku ya ufunguzi ya mashindano hayo Septemba 21 mwaka hu,  alitembelea kambi ya timu za Wizara hiyo jambo lililowapa wachezaji hamasa ya ushindi katika mashindano hayo.
Akizungumza na wachezaji hao katika kambi hiyo Naibu Katibu Mkuu  Gabriel aliwakumbusha mambo muhimu ya kuzingatia katika mashindano hayo hasa katika baadhi ya  masuala ya kiufundi kutokana na uzoefu alionao katika michezo kadhaa inachezwa katika mashindano hayo.
Pamoja na mambo mengine, Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara aliwataka wachezaji kuzingatia sheria za michezo husika bila ya kusahau nidhamu katika mashindano hayo ili kuhakikisha wanarejea na ushindi kwani Wizara hiyo ndiyo yenye dhamana na michezo nchini.
Mashindano hayo ya SHIMIWI yanaendelea katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma na Chuo Kikuu cha Dodoma na kushirikisha Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Makamtibu Tawala mkoa ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 5 mwaka huu.
Katika mchezo mwingine uliochezwa jana asubuhi timu za kuvuta kamba za Wizara ya Habari za wanaume na wanawake zimeshinda baada ya kuzifunga timu kamba kutoka  wakati za mpira wa miguu na pete zilitarajiwa kucheza mchana na jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...