Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Reginald Mengi akizungumza katika Mkutano uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam baina ya taasisi yake na Wizara ya Nishati na Madini kujadili suala la ushirikishwaji wananchi katika utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) Godfrey Simbeye akisoma tamko la taasisi hiyo kwa waandishi wa habari baada ya kikao chake na Wizara ya Nishati na Madini hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuhusu ushirikishwaji wananchi katika masuala yanayohusu utafutaji na uchimbaji gesi asilia.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika Mkutano baina ya Wizara na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mkutano ulikuwa ukijadili suala la ushirikishwaji wananchi katika utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) mara baada ya mkutano wao hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuhusu ushirikishwaji wananchi katika masuala yanayohusu utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia. Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Eliakim Maswi, Mwenyekiti wa TPSF, Reginald Mengi, Mkurugenzi wa Utafutaji, Uzalishaji na Shughuli za Kiufundi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. Emma Msaki, na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.


Dr Mengi tutakukumbuka kwa mchango wako thabiti.Wtatala wetu wajue hata hao matajiri wa dunia wenye uwezo wa gas walianzia mbali China inaonyesha maajabu kila mtu anajua historia yake,Prof awaombe tu msamaha watanzania kwa kuwakashfu kuwa wana uwezo wa kuwekeza kwenye machungwa tu.uwekezaji ni uwekezaji tu bora mitaji na akili ya kutawala mitaji ila ajue kuwa tunaweza.
ReplyDeleteDkt unafanya kazi mzuri m/mungu akulipe kwa juhudi za ktk kutafuta maendeleo kwa watanzania wenzako. Hatahivyo watanzania tungependa kupata ufafanuzi jinsi kuridhishwa kwenu juu ya ushirikishwaji huo kwani ni hivi karibuni tu tulishuhudia kutokubaliana kwenu na waziri mwenye zamana wa Nishati na Madini
ReplyDeletekuhusu ushirikishwaji wa wananchi
Mdau wa pili hapo juu nimeamini kuna wadau wengi tu wa blogu ya jamii ambao ni makini kufuatilia kila kitu kuhusu sasa TPSF a.k.a Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini ghafla bin-vuu kuridhishwa, je wameridhishwa na nini, mwenyekiti wa TPSF tunaomba taarifa kwa umma.
ReplyDeleteMdau
Taarifa + Data
Ukiona Bunda la Noti linaweza kudundulizwa kutokea Sarafu moja.
ReplyDeleteLa muhimu licha ya uwezo chini wa kihali wa Wananchi wa kawaida walio wengi pawepo na Fursa za uwekezaji endapo mtu anapohitaji na isiwe ni suala la watu Fulani!
Kumbukeni Mwanahisa ni mwanahisa hata kama ana uwezo wa kumiliki Hisa moja tu!
Niliwahi kumsikia ndugu yangu mmoja akisema ya kuwa hawezi kwenda Benki kufugnua Akaunti kwa kuwa ana amini kuwa na Akaunti au akiba Benki ni mpaka uwe na Mamilioni ya fedha kitu ambacho sio kweli, kwa kuwa hata hao wenye Mamilioni hii leo huwzi amini walianzia na Salio la mwanzo la kufungulia Akaunti tu!!!
JIFUNZENI UWEKEZAJI!
Tuombe Mungu hii Neema ya Mali (Gesi, Mafuta na Madini) isiwe Laana!
ReplyDelete