Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wanajeshi wa Tanzania nawapenda sana kwani mara zote hawahusudishi rushwa. Polisi ndio vinara wa hiyo kitu. Kazeni buti zoezi liendelee kila siku isiwe wakati operation tu. Wananchi tuko nyuma yenu.

    ReplyDelete
  2. Je haki za kina mama wa Kitanzania walioolewa na wageni waishio Tanzania kwa muda mrefu ni zipi?

    Maana taarifa inazungumzia tu kina mama wageni waishio isivyo halali Tanzania lakini wameolewa na Watanzania!

    Tunaomba ufafanuzi toka Operesheni Kimbunga.

    ReplyDelete
  3. Huu ufafanuzi una kasoro. Hivi mtu akipewa uraia kisha akazaa watoto nchini inakuwaje tena hawa watoto sio raia?? ufafanuzi gani huu tena. Naona nchi nyingi tu duniani once mtu akioa au kuolewa na raia wa nchi hiyo au kama alikuwa mkimbizi kisha akatuma maombi na kuwa raia na watoto wao wakazaliwa ndani ya nchi- automatically watoto hawa wanakuwa raia. It makes sense that way. Please make this more clear sio kuacha vitu vague. Tanzania inasifiwa kwa wema wake tangu kale na kale na tunataka rekodi hii tusipokonywe.

    ReplyDelete
  4. URAIA NA MAISHA UA UGENINI:

    Ndugu zetu Madiaspora wa Majuu wana uzoefu mzuri sana kuhusu Tasnia hii.

    Wanajua ni mshike mshike gani wanapata kutoka ktk Serikali za nchi walizopo, hivyo Waacheni Maafisa wa Serikali na Jeshi wafanye kazi yao.

    Mtu yeyote ambaye itatokea Uraia wake una utata, ni lazima ashughulikiwe na itakapo patikana uhakika wa suala lake, atapata haki yake na utaratibu utafuatwa!

    Je, mtakapo kosa haki zenu za kimsingi dhidi ya Wageni Haramu mnao wakingia kifua mtamlaumu nani?

    ReplyDelete
  5. Bora lawama kuliko fedheha!

    Hata kama watalalamika kototendewa haki, ni lazima watu walio na utata kuhusu Ukazi wao nchini washughulikiwe, kwa kuwa mara zote watu wa hali hizi huleta maafa makubwa ndio maana ktk nchi nyingi linapokuja suala la Uraia kunakuwa hakuna Msalie Mtume!!!,,,nchi zingine za Dunia unapigwa Repatriation ukaanze moja hukohuko kwenu kama utarudi ama utabaki moja kwa moja huko.

    Pia wapo Wapo Wageni haramu ambao wanatumia mwanya huu vibaya, wa kuwa na mazazi mmoja ama kuwa na mwenza mmoja Raia.

    ReplyDelete
  6. Ndugu zetu Afrika ya Mashariki:

    Hatuna roho mbaya isipokuwa tunataka EAST AFRICAN INTEGRATION ya kikweli na sio ya Kisanii.

    Msichukulie Tanzania kama Shamba la bibi kwa kukaa bila kufuata Sheria na Kanuni eti kisa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, mnatakiwe mfuate taratibu na ndio maana waliopo ktk Sheria hawakuguswa mmeguswa mliokuja miaka kibao mkawa mmejisahau na kuzaliana Ugenini kiholela na bila taratibu.

    UKAZI HARAMU NA MADHARA MAKUBWA KAMA TULIVYO SHUHUDIA NDUGU ZETU KUTOKA JAMHURI YA RWANDA WAKIISHI NCHINI KWA TIKETI YA UKIMBIZI HUKU KTK MADARI YA MAJUMBA YAO WAKIWA NA SILAHA KALI ZA KIVITA WAKIENDESHA SHUGHULI ZA UJAMBAZI, UPORAJI NA WIZI HAPA TANZANIA!!!

    HAKUNA INTEGRATIONA AMBAPO MKAZI RAIA ANATOLEWA KAFARA NA MGENI, HIYO HATA MATAIFA MAKUBWA KAMA MAREKANI WALIO MATAJIRI AMA SAUDI ARABIA HAWAKUBALI KAMWE.

    ReplyDelete
  7. Hawa wanaolalamika operesheni inamatatizo sio raia hao wachunguzeni Na wenyewe nahisi ni wale wachache wahamiaji waliobahatika kufanikiwa bongo sasa wanaona wachafue operesheni kimbunga aluta continua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...